Madereva Lusahunga Wataka Kumuona Rais Magufuli

Na Clavery Christian Biharamulo.

Kufuatia ajali za mara kwa mara katika barabara ya Lusahunga kwenda mpakani mwa Tanzania na Burundi baadhi ya madereva  wa magari makubwa ya  mizigo wameiomba  Serikali kuwatengenezea barabara hiyo ili kuwaondelea adha wanayokutana nayo.
kwa mujbi wa Madereva hao, kutokana na ubovu wa barabara hiyo wamekuwa wakilazimika kusafiri kwa kutumia saa nane mpaka kumi katika eneo la Lusahunga kwenda Benako kufuatia barabara hiyo kujaa mashimo makubwa yanayopelekea magari yao kuharibika vibaya na kuanguka na kuwasabishia ulemavu na wengine kupoteza maisha wanaopona hufukuzwa kazi na mabosi wao.

Barabara  ya Lusahunga  hadi  Lusumo  wilayani  Ngara mkoani Kagera inatumika kusafirisha bidhaa mbalimbali  kwa kutumia  malori makubwa  ya mzigo kwenda nje ya nchi licha ya barabara hiyo kuongeza pato la taifa imekuwa haipitiki kutokana na kuwa na makorongo na mashimo yanayopelekea magari kuanguka kwa kupata ajali zisizokuwa za lazima.
wakiongea na APC blog wamesema kuwa kufuatia ubovu wa barabara hiyo umepelekea  msongamano wa malori kupaki ovyo ovyo njiani kutokana na kupata kuharibika kwa magari hayo mengine yakianguka na kukata baadhi ya vyuma huku wakihofia usalama wa maisha yao na magari waliyo nayo kwani mda mwingine gari linaharibikia sehemu ambapo hakuna hata mtu yeyote wa kukupa msaada.
APC blog imefanikiwa kuzungumza na baadhi ya madereva  ambapo wametoa kilio chao na wengine wakiomba kukutana na Rais Dkt John Magufuli ili kumueleza kero ya barabara  hiyo  ambayo imekuwa sintofahamu kwao.
Mbali na madereva kulia na ubovu wa barabara hiyo  abiria wanaosafiri kutoka mikoa mbalimbali  kupita barabara hiyo  wamesema kuwa baadhi ya wamama wajawazito wamekuwa wakijifungulia kwenye gari  kabla ya muda wao kutokana na kurushwa rushwa kwenye mashimo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post