SAMATTA APIGA HAT-TRICK,KRC GENK IKIICHAPA 4-0 WAASLAND-BEVEREN UGENINI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amefunga mabao matatu peke yake, timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 4-0 katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji dhidi ya Waasland-Beveren Uwanja wa Freethielstadion mjini Beveren.
Samatta alifunga mabao yake yote kipindi cha pili katika dakika za 53, 66 na 86 baada ya. Paintsil kutangulia kufunga la kwanza dakika ya 21.
Huo unakuwa ushindi wa pili katika mechi nne za mwanzo za mabingwa hao watetezi, KRC Genk kwenye Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.

Kwa Samatta mwenye umri wa miaka 26 jana amefikisha mabao 66 ya kufunga katika mechi ya 160 katika mashindano yote tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika ligi ya Ubelgiji pekee amefunga mabao 51 kwenye mechi 126, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja na Europa League mechi 24 katika mabao 14.
Kikosi cha Waasland-Beveren kilikuwa: Gabriel, Wiegel, Caufriez, Vukotic, Vukcevic, Verreth, Buckets/Heymans dk67, Bizimana/Agyepong dk45, Schryvers, Badibanga na Forte/Sula dk62.
KRC Genk: Coucke, De Norre/Maehle dk70, Dewaest, Lucumi, Uronen, Berge, Heynen/Wouters dk86, Piotrowski/Hagi dk75, Ito, Paintsil na Samatta.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post