MKANDARASI AKABIDHIWA BARABARA YA BYPASS JIJI LA ARUSHA

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Halmashauri ya Jiji la Arusha limepata Fedha za nyongeza kiasi cha bilion 4,106 kwa ajili ya ujezi wa bar
Picha ya pamoja mara baada ya kukagua eneo la ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass itakayogharimu kiasi cha billion 4.106 hadi kukamilika mwezi januari mwakani picha na Ahmed Mahmoud Arush
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Kulanga akimkabidhi rasmi eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass Mkandarasi wa Ujenzi wa barabara hiyo Lang Shang ambaye ni mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro ya China  kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara nje kidogo ya jiji la Arusha leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Pichani ni Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay akisikiliza taarifa kutoka kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa pamoja na Mhandisi wa barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya makabidhiano hayo ya ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya jiji la Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Pichani ni Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay akisikiliza taarifa kutoka kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa pamoja na Mhandisi wa barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya makabidhiano hayo ya ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya jiji la Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
abara ya kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa 3.44 kupitia fedha za mradi wa TSCP inayoratibiwa na benki ya dunia chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi
Mradi huo ambao tarehe 27 mwezi huu umekabidhiwa na Halmashauri ya  Jiji la Arusha kwa Mkandarasi  Kampuni ya Ujenzi ya Snohydro ya nchini china utatekelezwa kwa muda wa miezi minne hadi Januari mwakani.
Akizungumza mara baada ya kuukabidhi mradi huo kwa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Kulanga ambaye pia ni Mwanasheria wa jiji hilo amesema kuwa mradi huo ni wanyongeza na utatekelewa ndani ya miezi minne.
Alisema kuwa mradi huo utasaidia kuondoa changamoto za msongamano katikati ya jiji la Arusha na una manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na utasaidia usalama kwenye uwanja mdogo wa ndege badala ya kukata katikati ya uwanja barabara hiyo itasaidia kuchepuka pembezoni mwa uwanja.
“Barabara hii ina umuhimu mkubwa sana katika uwanja wetu wa ndege na maeneo ya shule ya sekondari na itafungua fursa kwa wanaowahi katikati ya jiji kutoka stand kubwa ya mabasi ya mkoani inayotarajiwa kujengwa Olasit”
Kwa upande wake Mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro watakaojenga barabara hiyo Lang Yang Shang alisema kuwa wataifanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango vilivyowekwa na kwa ubora.
Alisema kuwa barabara hiyo na udogo ulipo hautawapa tabu kuikamilisha ndani ya wakati hivyo kuweza kukamilika bila kuwepo vikwazo vyovyote hivyo kuomba ushirikiano wakati wote wa ujenzi huo.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi  Agustini Mbuya alisema kuwa barabara hiyo ni muunganiko wa bypass na itarahisisha mchepuko na kusaidia usalama na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga fedha hizo.
Alisema kuwa mradi huo utaanza ujenzi rasmi tarehe 11 mwezi ujao na leo ndio makabidhiano kwa jiji kumkabidhi rasmi  mkarandari kwa ajili ya Ujenzi huo wa barabara
Nae Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alisema kuwa Barabara hiyo ni sehemu ya mkataba uliosainiwa wiki iliyopita na utakuwa kielelezo cha kueleza jinsi utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa wananchi mwaka ujao jinsi serikali ilivyotekeleza miradi.
Mwisho…..

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post