MOUNT MERU HOSPITAL YATANGAZA KAMBI YA MATIBABU BURE KUELEKEA MIAKA 100

Na, Egidia Vedasto, APC Media, Arusha.

Kuelekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanza kwa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha – Mount Meru, hospitali hiyo imetangaza kuendesha Kambi ya Matibabu Bure kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za maadhimisho hayo.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru, Dkt. Alex Ernest, amesema kambi hiyo itaanza Septemba Mosi, ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 100, na itafanyika katika viwanja vya hospitali hiyo.

Amesema katika kambi hiyo wananchi watapata huduma mbalimbali zikiwemo za uchunguzi na matibabu ya macho, uzinduzi wa namba kwa wagonjwa, huduma za matibabu kwa watoto pamoja na kampeni ya uchangiaji damu salama.

Dkt. Ernest amesema kampeni ya uchangiaji damu ni muhimu kutokana na mahitaji makubwa ya damu katika hospitali hiyo, ambayo kwa mwezi hufikia kati ya chupa 450 hadi 550.


Amesema Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru imepiga hatua kubwa katika uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukizwa, ikiwemo saratani, na kwamba hospitali hiyo inaongoza nchini miongoni mwa hospitali za rufaa katika huduma hizo.

Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya, hususan katika Hospitali ya Mount Meru, akisema uwekezaji huo umewezesha hospitali hiyo kuboresha huduma zake. Amesema mwaka 2020 hospitali hiyo ilipokea Shilingi bilioni 5.4 kwa ajili ya uendeshaji.

Dkt. Ernest amesema anajivunia mafanikio yaliyofikiwa na hospitali hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1926, kipindi cha ukoloni, ambapo awali ilitumika zaidi kutoa huduma kwa majeruhi, wakiwemo wanajeshi waliopigana katika Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia.

Amesema baada ya wakoloni kuondoka, wazawa waliendelea kutoa huduma kwa wakazi wa Arusha na kuendelea kuboresha huduma hizo, mwaka 2010, hospitali hiyo ilipandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha.


"Kuanzia mwaka 2020 kumekuwa na mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa sasa hospitali hii ina vifaa na mashine za kisasa za uchunguzi, ikiwemo vifaa vya uchunguzi wa saratani na endoscope, pamoja na madaktari bingwa takribani 40.

Ameeleza kuwa mafanikio mengine ni matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma, kuendesha kambi za matibabu katika maeneo ambayo wananchi wake hawafikiki kwa urahisi, kuweka mifumo ya huduma kwa wagonjwa pamoja na huduma ya kupiga simu bila malipo kwa wahudumu wa afya inayopatikana saa 24.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post