SERIKALI YARIDHISHWA NA UJENZI MIRADI YA UJENZI ARUSHA

Seif Mangwangi,  APC Media, Arusha. 

SERIKALI imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa katika Jiji la Arusha ikiwemo ujenzi wa stendi kuu ya mabasi katika eneo la Bondeni City, uwanja wa mpira kwaajili ya mashindano ya Afcon, soko la kilombero na bustani ya kupumzikia.


Akizungumza na Waandishi wa habari leo 18 Disemba 2025 ofisini kwake, Meya wa Jiji la Arusha amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe ametembelea miradi hiyo na kuongeza hatua iliyofikiwa.

Amesema Profesa shemdoe ambaye amefanya ukaguzi huo Leo Disemba 18,2025 na kuambatana na yeye Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amesema Serikali inapenda kuona miradi hiyo ikikamilika Kwa wakati.

Meya Iranghe amesema katika ukaguzi huo, Waziri shemdoe amesisitiza ufuatiliwaji wa karibu wa miradi hiyo na kusisitiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati. 

"Ujenzi wa soko la kilombero na stendi ya bondeni vinatakiwa kukamilika mwezi Mei 2026 sambamba na uwanja wa mpira unatakiwa kukamilika November 2026 ili kufanya maandalizi ya mashindano ya AFCON mwaka 2027, wananchi wana kiu ya maendeleo na wanataka mabadiliko ya haraka"amesema Prof.Shemdoe. 

Aidha Meya Iranghe amesema Waziri shemdoe ameelekeza baada ya soko la kilombero kukamilika wafanyabiashara waliokuwepo hapo mwanzo ndio wapewe kipaumbele kugawiwa vizimba na kwamba atafuatilia kwa karibu kuona utekelezaji wake.

"Nitoe maelekezo kwa Viongozi wa Jiji soko hili litakapofunguliwa tuhakikishe kwamba wale waliokuwa hapa mwanzo ndio wanapewa kipaumbele kwenye ugawaji wa vizimba na hili nitalifuatilia na kama kuna Afisa biashara atakwenda kinyume na hili kazi yake nitaondoka nayo.Niagize pia uwazi kwenye Vizimba vitakavyobaki nakemea tabia ya baadhi ya Viongozi kubeba vizimba na kukodisha kwa wananchi ili kupata cha ziada." Amesema Prof. Shemdoe.

Meya Iranqhe amesema wamepokea maelekezo hayo na kwamba Jiji litahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kusainiwa kwenye mkataba.

"Kipekee tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kututembelea, tuna imani naye na tunamshukuru Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za miradi ya maendeleo tunawahakikishia wananchi tutatimiza adhma hiyo.Nawaahidi wananchi mambo mazuri yanakuja" Amesema Iranqhe. 



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post