
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema leo kuwa Uturuki itawatuma
wanajeshi nchini Libya, kwa kuwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
imetoa ombi hilo.
Erdogan amesema atawasilisha mswada kuhusu ombi hilo katika bunge la Uturuki mwezi Januari.
Hapo
jana, Rais Erdogan aliizuru Tunisia kujadiliana na mwenyeji wake Rais
Kais Saied, kuhusu ushirikiano na uwezekano wa kusitisha machafuko
nchini Libya.
Kwenye
hotuba yake leo, Erdogan amesema Tunisia ilikubali kuiunga mkono
serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na inayoongozwa
na Fayez al-Serraj.