Waliofanya vizuri St Mary’s wapewa zawadi

Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim mwalimu wa shule ya sekondari St Mary’s Mbezi Beach Angel Focus,  baada ya shule hiyo kufanya vizuri kwenye mkitihani ya kidato cha nne kufanikiwa kutoa wanafunzi wengi wa daraja la kwanza na daraja la pili. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa bodi, John Kibona
Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim Makamu mkuu wa shule ya St Mary’s  Mbezi  Beach, Rajab Balele  kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim Mkuu wa taaluma wa St Mary’s Mbezi Beach High School, Shadrack Mgaya  baada ya shule hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka huu

Picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuriNa Mwandishi Wetu

WANAFUNZI waliomaliza  kidato cha nne kwenye shule ya sekondari St Mary’ s Mbezi Beach na kufaulu kwa daraja la kwanza wamepewa zawadi mbalimbali kama motisha kwa wanafunzi wengine kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.

Hafla ya kuwapongeza wanafunzi hao ilifanyika jana kwenye maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach na kuhudhuriwa na wazazi na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne.

Zawadi walizopewa wanafunzi hao ni pamoja na fedha taslim, nguo za michezo pamoja na vitabu mbalimbali vya kitaaluma.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Rajab Balele, alisema mwaka 2020 walimu waliahidi kuleta mageuzi makubwa na  walipambana usiku na mchana na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.


Alisema wanafunzi  106  wa shule hiyo walihitimu kidato cha nne mwaka jana na miongoni mwao, wanafunzi 29 walipata daraja la kwanza, daraja la II wanafunzi 35 wanafunzi 13 daraja la tatu na kwamba hakuna aliyepata sifuri.

“Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi wamefanyakazi kubwa sana usiku na mchana kuwa wabunifu kufundisha mpaka wanafunzi wengi kufaulu kwa alama za juu,” alisema na kuongeza.

“Nilipopata matokeo yetu ya kidato cha nne kwa kweli nilichanganyikiwa kwasababu sikuwa natarajia kwamba tutafaulisha kwa kiwango kikubwa namna hii, tulilahidi kufanya vizuri lakini matokeo yamekuwa mazuri sana kuliko nilivyotarajia,” alisema.

Balele aliwataka wanafunzi hao wasibweteke na badala yake waendelee kufanya vizuri kwenye elimu ya kidato cha tano na sita ili kupata alama zitakazowawezesha kujiunga na vyuo vikuu bila vikwazo.

 

“Kuna wakati shule ilikuwa hadi daraja 0 wanafikia wanafunzi 62 lakini kwa sasa hakuna division  0, na daraja la kwanza wameongezeka huu ndo mwaka tumefanikiwa kupata divisheni one nyingi kuliko mwaka wowote,” alisema na kuongeza.

“Kuna kufaulu na kufaulu sana, kwa hiyo ukiangalia matokeo yetu ya mwaka huu darala la kwanza za kiwango cha juu tumezipata nyingi na huo ndio utakuwa mwendo wetu tutahakikisha hakuna daraka 0 miaka yote na daraja la kwanza zitaendelea kuongezeka,” alisema.


Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Shadrack Mgaya, alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kitaaluma.

Alisema mafanikio ya wanafunzi yanategemea pembe tatu ambazo ni Mwalimu, Mwanafunzi na Mzazi ambapo kila mmoja anapotimiza wajibu wake matokeo yanakuwa  mazuri kama ambayo shule hiyo imepata kwa kidato cha nne.

 

 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post