MIILI 25, WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI NGARAMTONI KUAGWA KESHO SHEKHE AMRI ABEID.

 

Na Egidia Vedasto,

Arusha.


Shughuli ya kuaga miili ya watu  25 waliopoteza maisha katika ajali iliyohusisha Lori na magari madogo matatu iliyokea eneo la Ngaramtoni jijini Arusha inatarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa   shekhe Amri Abeid.


Akizungumza na waandishi wa habari  leo ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongera amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika shughuli  hiyo kwani inawagusa watanzania wote hata na dunia kwa ujumla.


Mongela ameeleza hayo wakati akipokea barua kutoka kwa viongozi wa waendesha daladala jijini Arusha wakitaka maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayotarajiwa kufanyika kesho 27 February,  kufanyika bila kubugudhi shughuli zingine za jamii.


"Naamini wenzetu wa CHADEMA  wanatambua jinsi msiba huu ni mzito kwa hiyo muwe na uvumivu  nina imani ni waungwana na  wataungana na sisi katika shughuli za kuaga badala ya kuandamana kwa siku ya kesho" ameeleza Mongela.


Ameendelea kusema kwamba "kama wataamua  wataandamana ulinzi upo na umeimarishwa kama siku zingine zote ila wasiingilie shughuli za jamii kukwama yaani kama ni daladala zifanye safari zao, wafanya biashara hivyohivyo wanafunzi ratiba zao zisiingiliwe" amesisitiza


"Vjiongozi wa dini na viongozi wengine wa serikali wameshauri watanzania wapate nafasi ya kuaga ndugu zao kama ishara ya upendo......miongozo ya jeshi la polisi iko makini na ulinzi umeimarishwa"


Kwa upande wa mmoja wa viongozi wa waendesha daladala jijini Arusha Dulla John ameiomba serikali kuwasaidia kufanya kazi zao kama siku zote kwani maisha ya watu wengi yanategemea mtu kutoka na kufanya kazi ili kujipatia riziki.


"Mimi ni dereva daladala nategemea kila siku kuwa barabarani ili nipate riziki na nimeajiriwa, vivyo hivo wafanyabiashara wadogo na wanafunzi wanatakiwa kwenda shule kwa kutumia daladala hizi tunazoziendesha, naomba msaada ili maandamano yasiingilie kazi zetu" ameomba dereva daladala John.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post