MKOA WA SHINYANGA WAZINDUA PROGRAM JUMUISHI YA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO


Na Moshi Ndugulile

Takribani watoto Milioni 250 wenye umri chini ya Miaka mitano katika Nchini zenye uchumi wa chini na kati wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu za ukuaji,kutokana na kukosa malezi bora

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye hotuba yake iliyowasilishwa na Mkuu wa wilaya ya kishapu Joseph Mkude, kwenye uzinduzi wa utekelezaji program jumuishi ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto,ambapo amesema takwimu zinaonyesha kuwa dunia nzima kuna takribani watoto milioni 250 kwenye nchi zenye uchumi wa chini na kati ambao wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua za ukuaji

Ameeleza kuwa takribani ¾ ya watoto wote sawa na 66% umri chini ya Miaka mitano waliopo kusini mwa jangwa la sahara wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu za ukuaji kutokana na kukosa malezi bora,umaskini,utapiamlo pamoja na matatizo mengine ya kiuchumi

Amesema hadi sasa Maendeleo ya awali ya Mtoto hayajapewa kipaumbele licha ya kwamba kipindi cha Miaka 0 hadi 8 ni fursa muhiu ya kuboresha Maendeleo ya binaadamu ili kupata mtaji bora wa raslimali watu wenye tija ,

Aidha kukosekana kwa fursa ya malezina Maendeleo ya awali ya mtoto katika umri huo (0-8) inaweza kusababisha changamoto katika maendeleo yao ambayo yanaweza kuathiri kizazi hadi kizazi

Kutokana na changmoto hizo na kwa kuzingatia umuhimu wa ukuaji na maendeleo ya  awali ya mtoto serikali imechukua hatua za kuondoa vikwazo vinavyokwamisha juhudi za malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMMMA) kwa kuandaa mkakati program jumuishi ya kitaifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM ya 2021/2022 hadi 2025/2026)

Akizungumza kwenye hafla ya kuzindua utekelezaji program hiyo Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanyanga Tedson Ngwale amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwekeza kwenye hatua za ukuaji wa Mtoto.

Serikali Mkoani Shinyanga imesema itaendelea kushirikiana na wadau wote kutekeleza afua zinazolenga kuchochea makuzi chanya,ya watoto ili kujenga taifa lenye watoto waliofikia utimilifu katika ukuaji, hatua ambayo imelenga kuandaa viongozi bora wa baadaye.

Uzinduzi wa program hiyo umehuduriwa na wadau mbali mbalimbali wa maendeleo likiwemo shirika la ICS ,AFYA PLUS,DOCTOR WITH AFRICA,TECDEN, WORD VISSION, Wamiliki wa shule binafsi na vituo vya kulelea watoto,SMAUJATA,maafisa maendeleo kata,ambapo Mkuu wa Mkoa Shinyanga Christina Mndeme ameyapongeza mashirika hayo kuunga mkono na kushiriki kikamilifu katika juhudi mbali mbali za serikali katika ustawi na maendeleo ya Mkoa na Taifa.

Utekelezaji wa program hiyo umelenga kuyafikia maeneo makuu matano ya kimkaati ambayo ni pamoja na upatikanaji wa afya bora ,lishe bora,malezi ya mwitikio,usalama na ulinzi wa mtoto na fursa za ujifunzaji wa awali.

Uzinduzi kwa ngazi ya Taifa ulifanyika Disemba 13,2021 huku kwa ngazi ya Mikoa awamu ya kwanza ilifanyika Mwaka 2022 katika Mikoa kumi ya awali,na baadaye Mwaka huu 2023 imefuatiwa na Mikoa 16 ukiwemo Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni  awamu ya piliThis is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post