MCHUNGAJI LUGEMBE AWAKUMBUSHA WAKRISTO KUSIMAMIA MISINGI YA MUNGU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mchungaji Charles Lugembe wa kanisa la AICT Kambarege mjini Shinyanga amewakumbusha wakristo kusimamia imani zao katika misingi  ya Mungu ili kuwa mfano bora wa kuigwa na jamii.

Ameyasema hayo leo Julai 23,2023 wakati akihubiri kwenye ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Kambarage ambapo amewasihi wakristo kuendelea kumcha Mungu katika misingi ya kweli.

Mchungaji Lugembe amewakumbusha wakristo kutokatishwa tamaa na changamoto za maisha hivyo amewasihi kusimamia imani zao kwa kuendelea kutenda matendo mema katika kuishi maisha ya kila siku.

Aidha ameongeza kuwa changamoto za maisha, migogoro pamoja na magonjwa isiwe chanzo cha kumuasi Mungu huku akiwasihi kuwa wavumilivu.

Baadhi ya waumini wa kanisa la AICT Kambarage wamemshukuru Mchungaji Lugembe kwa kufundisha somo hilo ambapo wamewaomba wakristo wengine kuendelea kumwamini Mungu ikiwa ni pamoja na kutenda matendo yanayompendeza.


Mchungaji Charles Lugembe wa kanisa la Africa Inland of Church Tanzania (AICT) Kambarege mjini Shinyanga akihubiri leo Julai 23,2023 katika ibada ya Jumapili.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post