SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA WAIKUMBUSHA JAMII KUTOA TAARIFA ZA UKATILI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imewaomba wakazi wa Mkoa huo kupaza sauti juu ya ukatili kwa kuripoti vitendo hivyo.

Hayo yamebainishwa na viongozi wa kampeni hiyo kwenye kikao cha kamati tendaji kilicholenga kujadili mambo mbalimbali ili kufanikisha shughuli za kupinga ukatili.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti idara ya wanawake Mwinjilisti  Ester Emmanuel amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutofumbia macho vitendo vya ukatili badala yake wanapaswa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika.

Kwa upande wake naibu katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Edson Sholagi amesema ipo mikakati mbalimbali ya kufanikisha kampeni hiyo ambapo wanatarajia kufanya ziara ya kutembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuibua ukatili na kuimarisha viongozi ngazi ya chini.

Naye katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya ametoa shukurani zake kwa kuteuliwa kutumikia nafasi hiyo huku akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa taratibu zilizopo pamoja na kushirikiana na viongozi wengine.

“Nashukuru sana kwa uteuzi wa Tarehe 24 Mwezi wa sita Mwaka huu 2023 kwanza kabisa nianze kumshukuru Mwenyekiti wangu ngazi ya Taifa Shujaa Sospeter Bulugu kwa kuniona na mimi kijana nafaa ambaye naweza kuchapa kazi nikiwa katibu wa Mkoa na mimi nitanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha tunapunguza au kumaliza kabisa ukatili, lakini pia nimshukuru waziri mwenye dhamana mama yetu Dkt. Dorothy Gwajima kwa kutambua mchango wetu sisi vijana”. Amesema Daniel Kapaya

“Lakini pia nimshukuru Mwenyekiti wangu wa Mkoa wa Shinyanga Madam Kisendi na waandamizi wengine nikiwa katibu wa SMAUJATA Mkoa nitashirikiana nao kwa karibu katika kufanya kazi hii kwa sababu tusipokuwa na ushirikiano maana yake tutashindwa kutokomeza ukatili, niseme tu kuwa nitajitahidi sana kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, kata, matawi mpaka watu wa chini kabisa tutawafikia ili kuibua ukatili unaoendelea kufanyika”. Amesema Daniel Kapaya

Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa shujaa Sospeter Bulugu alimteua Bwana Daniel Kapaya kuwa katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga tangu Jumamosi Juni 24,2023.

SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini iliyoanzishwa Mwaka jana chini ya Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Bwana Sospeter Mosewe Bulugu.

  

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akishukuru kwa kuteuliwa nafasi hayo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post