TCRA YATOA ELIMU KWA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA YAHIMIZA KUTUMIA TANZANITE PORTAL KWA HUDUMA ZA LESENI.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mhandisi wa  Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA  idara ya leseni na ufuatiliaji kitengo cha huduma kwa wateja Kadaya Baluhye amewaasa wadau wa mawasiliano ambao wanahudumiwa na mamlaka hiyo  kutumia mfumo wa Tanzanite Portal katika huduma za leseni.

Mhandisi Baluhye Ametoa wito huo Machi 31,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Hoteli ya Empire mjini Shinyanga wakati akitoa semina ya jinsi ya kutumia mfumo huo.

Mhandisi Baluhye amesema ni muhimu wadau wa mawasiliano ambao wanahudumiwa na TCRA kutumia mfumo huo katika huduma za kuomba leseni pamoja na kuhuhisha leseni zao.

Mhandisi Baluhye ametumia fursa  hiyo kuwataka wadau wa mawasiliano ambao wanahudumiwa na TCRA kufuata sheria na taratibu zilizopo katika uwekaji wa maudhui mtandaoni.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA leo imefanya semina fupi ya utoaji elimu kwa wadau wake jinsi ya utumiaji wa mfumo wa Tanzanite Portal kujisajili,kuomba na kuhuhisha leseni za mawasiliano.



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post