LHRC watoa msaada wa kisheria Singida mamia wajitokeza

 

Mwandishi wetu 


Arusha.Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu(LHRC) kimeanza kutoa bure ushauri wa kisheria  kwa wananchi wa mkoa wa Singida.Akizungumza na waandishi,Wakili Hamis Mayombo alisema zoezi hilo ambalo limeanza jumatatu wiki hii litakuwa la wiki moja.


Wakili Mayombo amesema hadi Sasa  mashauri mengi ambayo wamekuwa wakipokea ni migogoro ya ardhu,masuala ya mirathi na utawala bora, baadhi yatafikishwa mahakamani na mengine kupatiwa suluhu.


Wakili Mayombo ambaye ni Mkuu wa LHRC Ofisi ya Arusha,alisema mashauri ya ndoa yanatokana na migogoro ya kifamilia huku migogoro ya ardhi ikitokana na uvamizi wa ardhi.


Wakili w Fides Mwenda alisema baadhi ya mashauri ambayo wamepokea tayari yamefikishwa mahakamani na mengine bado.


"lakini pia kuna malalamiko ya viongozi kukiuka misingi ya utawala bora hivyo wamelalamikiwa"alisema


Mmoja wa Wananchi hao, Michael Itembe alisema anataka msaada wa kisheria kusaidiwa kupata shamba lake ambalo limevamiwa  na ndugu zake na kulima bila idhini yake.


"naomba LHRC isaidie kisitishwa kilimwa katika ardhi yangu hadi kesi ya msingi imalizike"alisema


LHRC itatoa huduma za kisheria kwa wiki moja mkoani Singida.


Jumanne Issa alieleza kuvamia ardhi yake na tayari shauri limefishwa mahakama I lakini hata hivyo bado suluhu haijapatikana.


Rehema Peter mkazi wilaya ya Ikungi alieleza kusumbuliwa na ndugu wa marehemu mume wake katika suala la mirathi kwani wanataka kunyang'a ya Mali zake


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post