Askofu Sangu akemea matapeli wanaotumia matatizo ya wengine kujinufaisha

 Na Simeo Makoba, Shinyanga


Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia shida na matatizo ya wengine kama fursa ya  kujinufaisha wao badala ya kuwasaidia wenye uhitaji.Akizungumza kupitia Misa ya Dominika ya Matawi ambayo imefanyika jana Jumapili katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga,Askofu Sangu amewataka wanaofanya vitendo hivyo kuacha kuwaongezea maumivu watu walioko katika mahangaiko ya namna mbalimbali na badala yake waongozwe na moyo wa utu, huruma na upendo na kuwasaidia kadri ya mahitaji yao .”Na kwamwe tusitumie shida na mahangaiko ya wengine kwa lengo la kujinufaisha,mfano zipo NGO’S nyingi sana ndani ya nchi yetu lakini ukiangalia kwa undani kabisa si kwa ajili ya watu wenye mateso na wenye mahangaiko na badala yake kinachowafikia walengwa ni asilimia ndogo ya raslimali zinazotolewa na wahisani,kiasi kikubwa kinatumika kwa ajili ya watu kujinufaisha kupitia shida zao”.Askofu Sangu pia ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza Wakristo wote kuepuka dhuluma na kutokuwa chimbuko la mateso kwa wengine na badala yake  wahakikishe wanakuwa chimbuko la matumaini na faraja kwa watu wenye shida.Leo,Kanisa Katoliki kote ulimwenguni linaadhimisha Dominika ya Matawi ambayo ni kumbukumbu ya kupokelewa kwa Shangwe kwa Yesu Kristo mjini Yelusalemu,tukio lililofanyika siku chache kabla ya kukamatwa kwake,kuteswa na kufa msalabani na baadaye kufufuka siku ya tatu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post