Waziri Mchengerwa aripoti Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo


Na Eleuteri Mangi, WUSM-Dodoma Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameripoti Ofisini kwake Mji wa Serikali Mtumba mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.Mhe. Mchengerwa amepokelewa na watumishi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi tayari kwa kuanza kazi ambayo Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Januari 8, 2022 kushika wadhifa huo.Uteuzi wa Mhe. Mchengerwa unafuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambayo ameyafanya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan siku ya Jumamosi na kuapishwa Januari 10, 2022 kushika wadhifa huo na kuchukua nafasi ya Waziri Innocent Bashungwa ambaye amehamishiwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).Aidha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Said Othman Yakubu pia ameripoti wizarani hapo tayari kutekeleza majukumu yake ikiwemo kusimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ambazo ni nguvu laini (soft power) ya taifa na sekta zinazowapa furaha Watanzania.Katika hafla hiyo ya kuwaapisha viongozi, Mhe. Rais amewaapisha pia Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post