Wakazi Shinyanga watakiwa kuonyesha ushirikiano ktk maduka ya maendeleo

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Diwani wa kata ya  Mjini katika Manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Abubakari amewataka wananchi hasa vijana kuendelea kuonyesha ushirikiano katika masuala ya maendeleo ya jamii kwa lengo la kujenga Jamii endelevu.


Ametoa rai hiyo wakati wa zoezi la upandaji miti ambalo limefanyika katika kata hiyo na kuwezesha idadi ya miti 261 kupandwa kwa siku moja na kueleza kuwa ni vyema kwa wananchi kutunza mazingira kwa gharama yoyote ili kuepukana na athari za ukame zinazoweza kujitokeza.


“Miaka 60 iliyopita na miaka 60 hii iliyopo mika ile ya nyuma kulikuwa kuna neema kuwa watu tulikuwa tunalinda miti lakini sasa hivi sisi tumekuwa tunakata miti na tunapokata hatupandi miti hii imekuwa ni shida ndiyo maana tumekuwa tunafukuzia ukame wakati mwingine mazingira tukitaka tuyadumishe tusitegemee tu kwamba mvua tufanye mvua iwepo isiwepo lakini sisi tupande miti na tumwagili ili kusudi tulete mandhari ya miji yetu kuwa ya kijani naamini tukifanya hivyo tutaendelea vizuri na mazingira yetu yatapendeza” Amesema diwani Abubakari. 


Aidha Diwani Abubakari ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kujenga Taifa lenye maendeleo kwa manufaa ya wananchi.


“Mimi niombe tumuunge mkono mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki anachokiongoza yeye kwa matukio yote anayofanya ambayo ni mabadiliko ya nchi  ili sisi tulete mabadiliko ya mazingira na mazingira haya tutaleta mabadiliko kwamba tukilinda hali ya miti iliyopo na kupanda miti kwa wingi tumuunge mkono kwa hali na mali tusimbeze hata kidogo yeye ndiye mfalme wetu, kiongozi wetu na yeye ndiye Rais wetu ilikusudi tulete maendeleo kwa pamoja hakuna linaloshindikana bila kuwa na umoja”.


Kampeini ya upangaji miti inaendelea kutekelezwa katika kata na Mitaa mbalimbali mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kukabiliana na Janga la ukame linalopelekea athari mbalimbali kwa wananchi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post