SIDO Shinyanga yawajengea uwezo vijana 71

Vijana 71 wakiwa wameshikilia vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali kutoka Sido

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga lililopo katika Manispaa ya Shinyanga  leo limehitimisha mafunzo kwa vijana 71 yaliyolenga kuwapatia ujuzi na maarifa vijana hao ili kutengeneza  ajira.


Mafunzo hayo yaliaza Novemba 4 mwaka huu 2021 ambapo jumla ya wanawake ni 25 huku wanaume ni 46 ambao wote umri wao ni kuazia miaka 18 hadi 35


Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo, Meneja wa shirika hilo Hopeness Kweka amesema mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa siku 16 yatawapatia vijana hao vipato pamoja na kuchangia Katika uchumi wataifa.


Meneja Kweka amesema shirika la SIDO litahakikisha vijana hao wanafanya kazi kadri walivyojifunza ili wasirudi nyuma na waweze kupata maarifa zaidi ambayo yatafanikisha kutimiza ndoto zao za kimaisha.


”Vijana hawa tunategemea baada ya kupata mafunzo haya na ujuzi huu wataenda kujiajiri na kutengezea ajira kwa watu wengine na rai yetu kuona lengo la mradi kama lilivyoandikwa kwamba ni kuwapa elimu na ujuzi ili wakatengeneze ajira kwao lengo la msingi  ni kutengeneza vipato kwao, familia zao pamoja na kuchangia maendeleo au uchumi wa nchi yetu wasiwetegemezi kwenye familia zao na kazi ya sido itakuwa ni kuendelea kuwafuatilia kuhakikisha kwamba vijana hawa wanatekeleka kadri walivyojifunza ili wasirudi nyuma”


Mgeni rasmi katika hafla hiyo katibu tawala wa wilaya ya shinyanga Bwana Boniphace Chambi ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya shinyanga amewapongeza wahitimu hao kwa kupata fursa hiyo ya kufundishwa kwa vitendo bila gharama. 


Bwana Chambi amewataka wahitimu hao kuitumia vizuri elimu hiyo waliyoipata ili waendelee kujiongezea ujuzi zaidi kuliko kukaa nyumbani.


“Ile elimu ambayo tumeipata hapa tukaifanyie kazi kadri tunavyofanya kazi ujuzi unaongezeka lakini ukienda kulala tu ujuzi utapotea kila mmoja kwenye kata yake kuna afisa maendelea ya jamii ukienda kwenye kata nenda kwa afisa maendeleo ya jamii mwambie hivi mimi nina ujuzi huu lakini sina uwezo wa kupata mtaji utanisaidiaje atakupa maelekezo maelekezo moja wapo ni kujiunga kwenye vikundi ili kupewa mkopo zamani walikuwa ni watu kumi sasahivi ni watano tu mnapata mkopo”   


Kwa upande wao baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo hayo wamelishukuru shirika hilo la SIDO kwa kuwapatia mafunzo hayo ya vitendo ambayo yatawasaidia kujikimu na kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakumba ikiwemo ukosefu wa ajira.


Mafunzo hayo ni Ushonaji, Utengenezaji wa magari, Uchomeleaji, Utengenezaji wa Keki, Mikate na Sikonchi pamoja na Utengenezaji wa bidhaa za ushonaji Viatu, Mikanda na Sendo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post