Kiwanda cha AtoZ chakabidhi msaada wa darasa sekondari ya Mateves

Mkurugenzi uzalishaji wa kiwanda cha AtoZ, Binesh Harria pamoja na familia ya Shah wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya darasa hilo


 * Mkurugenzi akubali kuwa mlezi wa shule

*Atoa ahadi nyingine ya msaada ujenzi wa matundu 6 ya choo

Na Seif Mangwangi, Arusha

Kiwanda cha A to Z kupitia  kumbukumbu ya marehemu Vilas J Shah na Nathalal Hirj Shah imekabidhi Halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru msaada wa darasa moja lililokamilika kama moja ya misaada ambayo imekuwa ikitolewa na kiwanda hicho kwa jamii.

Mkurugenzi uzalishaji wa kiwanda cha AtoZ, Binesh Harria pamoja na familia ya Shah wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya darasa hilo


Darasa hilo lililojengwa kwa gharama yazaidi ya Tsh Milion20 katika shule ya sekondari Mateves, limekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Selemani Msumi.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa  uzalishaji wa kiwanda cha AtoZ Textile Mills, Binesh Haria, msaada huo unatokana na uwajibikaji wa kiwanda kwa jamii (Community responsibility), katika kusaidia miradi ya maendeleo na kwamba fedha za ujenzi wa darasa hilo umetokana na faida kidogo ambayo imepatikana kutoka na uzalishahi kiwandani hapo.

Wanafunzi sekondari nya Mateves walimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha
Diwani wa kata ya Mateves Fredy Lukumay
viongozi wa CCM wakiwa katika halfa hiyo
Wanafunzi wa sekondari ya Mateves wakisoma risala kwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhiwa darasa na kiwanda cha AtoZ


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Selemani Msumi ametoa wito kwa taasisi na kampuni mbalimbali zilizoko wilaya ya Arusha kuiga mfano mzuri ulioonyeshwa na uongozi wa kiwanda cha AtoZ kusaidia Serikali ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali kwa manufaa ya jamii.


Amesema maendeleo ya wananchi yanategemea wadau mbalimbali na sio serikali pekee kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakitafakari hivyo.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mateves Fred Lukumay amesema kiwanda cha A to Z kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii inayoizunguka na kwamba ujenzi wa darasa hilo moja ni miongoni mwao misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na kiwanda kwa jamii.


Wakati huo huo, Binesh amekubali ombi la uongozi wa shule ya sekondari matevezi la kuwa mlezi wa shule hiyo sanjari na kuahidi kujenga matundu sita ya choo kutokana na shule hiyo kukabiliwa na upungufu wa matundu 16.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post