SERIKALI YAAGIZA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI KUTOA AJIRA VIJIJINI

 

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 01/08/2021 katika Kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akitoa maagizo kwa wakandarasi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha kuwa kifaa mbadala cha wiring UMETA kinapatikana ili wananchi wasiomudu gharama za wiring waweze kuvitumia kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge akiongea na umati wa wananchi wa Kijiji cha Nalasi kilichopo Wilaya ya Tunduru ambako uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 01/08/2021.

Watoto wakifuatilia matukio ya uzinduzi.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwakabidhi wazee kifaa cha UMETA ambacho ni mbadala wa wiring ili waweze kuunganishiwa umeme katika nyumba zao.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Ruvuma Brigedia Jenerali,Balozi Wilbert Ibuge pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Agosti 1,2021.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Ruvuma Brigedia Jenerali,Balozi Wilbert Ibuge pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga Makofi mara baada ya kuzindua Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Agosti 1,2021.

………………………………….

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini kutoa kipaumbele cha ajira kwa vijana waliopo katika vijiji ambapo miradi hiyo inatekelezwa.

Dkt. Kalemani alitoa agizo  wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Agosti 1,2021 katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru.

“Wakandarasi chukueni vibarua kutoka katika vijiji ambavyo mnapeleka umeme” alisema na kuongeza kuwa lengo ni kufanya miradi hiyo iwe na tija kwa kuwashirikisha wananchi katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.

Aidha, Mhe. Kalemani amesema Serikali itatumia zaidi ya Shilingi bilioni 71 kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vijiji 265 ambavyo havina huduma ya nishati hiyo katika Mkoa wa Ruvuma.

“Katika Mkoa wa Rvuma, vijiji vyenye umeme ni 289 kati ya 554. Kwa kutambua hilo leo ninawakabidhi wakandarasi waushambulie Mkoa wa Ruuma na kuhakikisha vijiji vyote vilivyosalia 265 vinapatiwa umeme kupitia mradi huu. Nipende kutoa rai kwa Watanzania wote kuwa kila Mtanzania atapata Nishati ya Umeme” alisema Waziri Kalemani.

Waziri Kalemani alisema kuwa Wilaya ya Tunduru ambako Mradi umezinduliwa kuna vijiji 85 ambavyo hadi sasa bado havijafikiwa na huduma ya umeme na kwa kutambua hilo, Serikali imetenga  takribani Shilingi bilioni 23.52 kwa ajili ya kuvifikishia umeme vijiji hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge aliwataka wananchi wasihujumu miundombinu ya kusambaza umeme kwa kuiba nyaya na vifaa vingine na wawe walinzi wa miundombinu hiyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post