DC Kilosa aongoza zoezi la kuchanja chanjo ya Uviko19

Kilosa, Morogoro

Serikali  imeendelea kuchukua hatua ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini kwa kutoa elimu ya afya kwa jamii ili iweze kuchukua tahadhari za kujikinga pamoja na  kuendelea kusambaza chanjo kwa jamii ili kudhibiti ugonjwa huo.

Akizungumza katika zoezi la  uzinduzi wa chanjo hiyo kwa Wilaya ya Kilosa, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaj Majid Mwanga amesema chanjo hizo ni salama na bora kwa ugonjwa wa virusi vya uviko 19 na imethibitishwa kimataifa na katika maabara zetu nchini.

 Amesema chanjo hiyo ni bora kwasababu ina uwezo wa kumpatia kinga mtu aliyechanjwa asiweze kufariki dunia endapo itatokea kaambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

" Ndugu zangu chanjo hii ni salama kwa asilimia 100, ni chanjo yenye lengo la kupambana na virusi vya covid-19,  inalenga kupunguza vifo vitokanavyo na korona pamoja na kupunguza maambukizi,"amesema.

Alhaji Majid ameitaka jamii kuepukana na taarifa zisizo rasmi kuhusu chanjo hiyo ikiwemo  maneno ya mitaani kwamba chanjo hiyo ina madhara jambo ambalo si kweli kwani zimefanyiwa tafiti na kuitaka jamii kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo kwa ajili ya afya zao.

Akisoma taarifa ya chanjo ya uviko 19 Mratibu wa Chanjo Msaidizi, wilaya ya Kilosa James Olomi amesema Wilaya imepokea jumla ya dozi 4000 ambazo zimesambazwa katika vituo vilivyoteuliwa kwa ajili ya kutoa chanjo katika zahanati ya Dumila, hospitali ya Wilaya  na kituo cha Afya Mikumi.

Amesema ugonjwa huo upo katika ngazi ya jamii hivyo ipo haja ya jamii kuendelea kuchukua tahadhari hususani katika maeneo ya mikusanyiko pamoja na kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kusitisha ama kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.


Pamoja na hayo Ulomi amesema makundi hatarishi ni pamoja na watumishi wa afya, watumishi wanaohudumia jamii kwa kukutana na watu mbalimbali, watu walio na umri zaidi ya miaka 50 na wale wenye magonjwa sugu mfano kisukari na presha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post