SERIKALI YAKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI 98,048,000 KWA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI WA MAZAO YA MISITU HANDENI

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa nne kulia) na Balozi wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa tatu kulia) wakikabidhi mavazi na buti kwa kikundi cha wajasiriamali cha Uhunzi wa Majiko Sanifu katika hafla fupi ya kukabidhivifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa pili kulia) na Balozi wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa kwanza kulia) wakikabidhi mojawapo ya mzinga wa nyuki kati ya mizinga 529 kwa kikundi cha wajasiriamali cha ufugaji nyuki katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akihutubia wananchi katika hafla fupi ya kukabidhivifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa sita kulia) na Balozi wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa tano kulia) wakikabidhi mashine ya kuchakata mbao kwa kikundi cha wajasiriamali cha uselemala katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga. Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ambaye ni Mkuu wa Wilaa ya Handeni, Mhe. Siriel Mchemba(wa nne kulia).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa kwanza kushoto) na Balozi wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa pili kushoto) wakikabidhi mashine ya kufua umeme kwa kikundi cha wajasiriamali cha uselemala katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga. Anayeshuhudia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaa ya Handeni, Mhe. Siriel Mchemba(katikati).

Baadhi ya wananchi wa vijiji vya Wilaya ya Handeni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akihutubia katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Ezekiel Mwakalukwa akitoa maelezo kuhusu uanzishwaji wa mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (FORVAC) katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

**************************

Na Happiness Shayo-Handeni

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa vikundi 20 vya wajasiriamali vinavyojihusisha na ufugaji nyuki, seremala, uhunzi wa majiko banifu kutoka vijiji vya Mazingara, Kitumbi, Gole, Kwamsundi na Kwedikabu Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Mhe. Masanja amesema kuwa makabidhiano hayo ni mwendelezo wa awamu za ugawaji vifaa kwa wanavijiji ili kuinua uchumi wao.

 “Awamu ya kwanza ilifanyika mwezi Machi, 2021 kwa wananchi wa Wilaya ya Songea Mjini, Namtumbo na Ruangwa ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) alikabidhi mashine tatu za kisasa za kuchakata magogo” amesema Mhe. Masanja.

Amefafanua kuwa vifaa hivyo vyenye gharama ya shilingi 98,048,000 ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (FORVAC)  ambao pamoja na mambo mengine unaangalia namna bora ya kutumia mazao ya misitu katika hali ya uendelevu.

Aidha, amewataka wajasiriamali hao kuhakikisha wanatumia vizuri vifaa walivyokabidhiwa  ili viweze kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuongeza mapato kwa wananchi.

Naye, Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan amesema mradi wa FORVAC nchini Tanzania ulianza mwaka 2018 ukiwa ni moja ya miradi mikubwa inayosaidia kukuza ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Finland.

Amesema lengo la mradi huo ni kuongeza mapato ya kiuchumi, kijamii na kimazingira kiutokana na misitu inayopatikana nchini Tanzania.

Balozi Swan ametaja mikoa ambayo mradi huo umekuwa ukitekelezwa kuwa ni Tanga, Ruvuma, Lindi na Dodoma .

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ilianzisha mradi wa FORVAC kwa lengo la kusaidia wananchi kuanzisha na kumiliki misitu ya vijiji kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kuwa baada ya wananchi hao kumiliki misitu hiyo, watumie fursa hiyo kuvuna rasilimali iliyopo kwa njia endelevu ili kukuza uchumi wao.

Hafla ya ugawaji vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo ilihudhuriwa na Viongozi kutoka Mkoa wa Tanga, Viongozi na Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Viongozi na Watendaji kutoka FORVAC na wanavijiji wa Wilaya ya Handeni

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post