TIGO WAKAMILISHA KUKABIDHI HUNDI ZA MAMILIONI YA PESA KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHEHEREKEA PESA

  Na Mwandishi Wetu

Mtandao namba moja wa Kidigitali hapa nchini Tigo, umeendelea kukabidhi Hundi za Milioni Kumi kumi kwa baadhi ya Washindi 10 wa Droo ya Mwisho ya Sheherekea Pesa na Tigo Pesa, washindi hao walipatikana Katika mikoa mbalimbali hapa nchini na tiyari watano Kati ya hao waliopatikana Jijini Dar Es Salaam wameshakabidhiwa Hundi zao.

Ikumbukwe kuwa June 3, 2021 Droo kubwa ya kuwapata washindi wa Jumla Wa Shilingi milioni 100 ilichezeshwa Makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaaam. Ambapo siku ya tarehe 8, June 2021 washindi wawili ambao ni Mandela Charles Erio Mkazi wa Tangi Bovu Jijini Dar Es Salaam na Lucy P. Komu
Mkazi wa Sinza walikabidhiwa Hundi ya milioni Kumi kumi kila mmoja Rasmi na kupata nafasi ya kuwapongeza Tigo Kwa kusheherekea miaka 10 kwa kuwajali wateja wake.

 

Lakini pia walielezea kwa namna gani wameweza kuibuka washindi wa hizo milioni 10 , ambapo walisema kuwa Siri pekee ilikua ni kufanya miamala mbalimbali Kama kununua LUKU, kulipa Bili na kufanya malipo mbalimbali ya Kiserikali kwa kutumia Tigo Pesa.

Zoezi liliendelea tena, ambapo Jana Juni 9, zoezi la kukabidhi Hundi hizo limefanyika kwa Washindi wengine wawili wa Million Kumi Kumi ambao ni Bi. Kachughu Msemo Huyu ni Mama Lishe anapatikana Segerea Jijini Dar Es Salaam na Domina G. Baryune huyu ni Karani anaishi Kivule Ccm Jijini Dar Es Salaam

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Hundi iyo Bi. Kachughu amewapongeza sana Tigo kwanza kwa Kutimiza miaka 10 ya Tigo Pesa lakini pia kwa Ofa na Huduma nzuri wanazotoa kwa Wateja wao

 

" Kwakweli Miaka hii 10 ya Tigo Pesa inaenda kubadilisha maisha yangu, maana hii milioni 10 niliyoishinda itanisaidia kuboresha biashara yangu maana Kama mnavyoona Mimi ni Mama Lishe nauza Supu lakini pia naenda Kuongezea vyumba viwili katika nyumba yangu " Alisema Bi. Kachughu huku akilengwalengwa na machozi ya Furaha .

Kwa upande mwingine Bi. Domina ambaye yeye ni Karani ameanza kwa kuwashukuru Tigo Kwa hizo milioni 10 walizomkabidhi na kusema kuwa anayo mengi ya kuifanyia hela iyo aliyoshinda ikiwemo kuanza mradi wa Kufuga kuku wa Kisasa.

Na hatimaye Leo Tarehe 10, June mshindi mwingine wa Tano, Bi. Pendo A. Mushi mfanyabiashara ya Saluni Ndani ya Jiji la Dar Es Salaam amekabidhiwa Hundi yake ya Million 10.

Kumbuka hao ni baadhi Kati ya washindi 10 wa Droo Kubwa ya Sheherekea Pesa na Tigo Pesa ambao waliibuka washindi baada ya kufanya miamala zaidi kwa kutumia Tigo Pesa

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post