DC Kilosa Alhaj Majid Mwanga asifu jitihada za Waziri Kabudi kujali elimu ya mtoto wa kike

 Na Mwandishi Wetu, Kilosa

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Hemed Mwanga amempongeza mbunge wa jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi kwa juhudi zake alizozionyesha kama kiongozi kwa kufanya jambo linaloacha alama katika jamii kwa kujali elimu ya mtoto wa kike baada ya kuandaa kambi ya mafunzo kwa mtoto wa kike. 

Pongezi hizo amezitoa leo alipotembelea kambi ya watoto hao na kujionea namna watoto hao wanavyojifunza mambo mbalimbali ikiwemo masomo ya sayansi, hisabati, kiingereza, stadi za maisha na elimu ya UKIMWI.

 


Mwanga amesema hilo ni wazo zuri linalopaswa kuwa endelevu kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia watoto wa kike kujitambua, kujithamini na kujiamini hatimaye kufikia ndoto zao.


Aidha amewataka wanafunzi hao wa kidato cha kwanza hadi cha tatu wapatao 220 toka shule 22 za kata toka jimbo la Kilosa kuwa mabalozi wazuri wa kuigwa pindi watakaporudi mashuleni jambo litakalowasaidia kutimiza ndoto zao kwani uzuri wa mtoto wa kike ni kichwa chake huku akiahidi kushughulika na wale wote watakaobainika kuwa kizuizi cha mtoto wa kike kutotimiza ndoto zake.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post