Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul amekutana na
Waigizaji waliohitimu mafunzo ya uigizaji chini ya udhamini wa Kampuni
ya MultChoice Bungeni Jijini Dodoma Mei 6, 2021.
Mheshimiwa Gekul amewataka waigizaji hao kutumia taaluma waliyoipata kuboresha kazi zao ili kuuza kazi zao ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa kazi za wahitimu hao ni tamthilia ya Jua Kali, Huba na Pazia ambazo zinaonyeshwa kupitia Chaneli ya Maisha Magic Bongo ya Dstv.