DIT WAVUNJA REKODI NYINGINE TENA DODOMA , MAONESHO YA PILI YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

 Na Mwandishi Wetu. 


Ikumbukwe kuwa maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yalizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  Ijumaa ya Mei 28, 2021 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na kama ilivyo kawaida siku zote Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaaam (DIT) ilishiriki katika maonesho hayo na kuonyesha bunifu mbalimbali zilizobuniwa na kutengenezwa ndani ya Taasisi hiyo. 

Viongozi mbalimbali wa serikali walitembelea na kuona bunifu mbalimbali zilizofanyika ndani ya Taasisi hiyo, moja kati ya viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.  Anthony Mtaka ambaye alifika na kujionea bunifu mbalimbali ikiwemo Taa za barabarani za kuongezea magari na za kuruhusu  wavuka kwa miguu zilizobuniwa na kutengenezwa na DIT kupitia Kampuni Tanzu ya Taasisi hiyo (DIT Company Ltd).

Mtaka alipongeza teknolojia hiyo na akaahidi kufanya mazungumzo na DIT ili zifungwe pia katika jiji la Dodoma kama mbavyo zimefungwa Mkoani Simiyu.

"Hizi taa nazifahamu vizuri tumezifunga kule Simiyu na ni mimi niliwakaribisha kule  mje tuzungumze tuone namna zifungwe pia hapa Dodoma," anasema Mtaka ambaye alikua Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kabla hajahamishiwa Dodoma na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Mtaka alisema anapenda kuona bunifu mbalimbali zinazobuniwa na vijana zinaboreshwa na kuingia sokoni kwenda kutatua changamoto katika jamii na si kuishia vyuoni.

Kazi kubwa ya Kampuni Tanzu ya DIT ni kubiasharisha bunifu zinazobuniwa katika Taasisi hiyo na kuzipeleka sokoni kama ilivyo taa hizo za barabarani. 

Bunifu nyingine ambazo zimeingizwa sokoni na Kampuni hiyo ni pamoja na mashine ya kutengeneza chakula cha samaki, bidhaa za ngozi kama vile mikanda, viatu na mabegi, kiti cha kuchaji cha walemavu, kiwanda kinachotembea ambacho kinamfa mkulima alipo kinapukuchua mahindi, kusaga nafaka aina zote, kuvuta maji na kubeba mizigo.


Mashine ya kuuza maziwa kwa mteja kujihudumia mwenyewe, ambapo mnunuaji anaingiza sarafu na maziwa yanatoka

Taa za barabarani za kuongezea magari na za kuruhusu  wavuka kwa miguu zilizobuniwa na kutengenezwa na DIT kupitia Kampuni Tanzu ya Taasisi hiyo (DIT Company Ltd).
                                                               Kiwanda kinachotembea

Kifaa cha kukusanya taarifa yahali ya hewana kutuma ujumbe kwa wakulima kimebuniwa na Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post