TIGO WAOMBA RADHI, WATANGAZA BONGE LA OFA KWA WATEJA WAKE

 Tunapenda kuwajulisha wateja wetu wa Tigo Pesa kuwa huduma zetu za Tigo Pesa zimerudi hewani na wateja wetu wanaweza kuendelea kufurahia huduma hizi baada ya kukosekana kutokana na tatizo la kiufundi. Tunatambua umuhimu wa huduma zetu katika kurahisisha shughuli zetu za kila siku hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.


                                    Angelica Pesha-Afisa Mkuu wa kitengo cha Tigo Pesa


Vile vile, nichukue fursa hii kuwahakikishia wateja wote wa Tigo Pesa kuwa fedha zenu zote ziko salama kabisa.


 


Tunawashukuru wateja wetu wote kwa uvumilivu na utulivu walioonyesha katika kipindi hiki, hivyo basi tunatoa ofa kabambe kama shukrani kwa wateja wetu. Ofa hii itahuisisha;


Kutuma Pesa bure kwa wateja wa Tigo Kwenda Tigo

Hakutakuwa na gharama za kufanya miamala ya Lipa kwa Simu katika maeneo yote ambapo huduma hii inapatikana

Kuhamisha pesa kutoka benki kwenda kwenye akaunti ya Tigo Pesa kuanzia shs 100,000/ utapata bonus ya hadi shs 20,000/- kwa wateja wote nchi nzima

Ofa hii ni kuanzia leo tarehe 8/April hadi Jumapili tarehe 10th April.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post