KAMPENI YA "NOGESHA VALENTINE NA ITEL" YAZINDULIWA, ZAWADI KIBAO KUTOLEWA

 Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya itel imezindua kampeni ya promosheni ya ‘Nogesha Valentine na itel’  jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam meneja mahusiano wa itel Bw. Fernando Wolle amesema  lengo la kampeni hiyo ni kuonesha upendo kwa wateja wake pamoja na kuwapa nafasi wateja waoneshe upendo kwa wale wanaowapenda.


“Ndio maana kampeni ya promosheni hii tumeita Nogesha Valentine na itel kwasababu kuna zawadi nyingi za kunogesha valentine kwa kila mteja atakayenunua simu ya itel na hasa mteja atakayenunua itel S16, itel A56 au itel A35 ataingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda zawadi kubwa kama vile TV ya itel yenye inch 43, inchi 32, simu, na mshindi mkubwa zaidi kupata nafasi ya kwenda hotel kubwa ya kifahari na ampendaye kwaajili ya Valentine Dinner” Amesema Wolle.

Wolle ameongeza kuwa droo kubwa  itachezeshwa mara tatu na kila droo itakuwa na zawadi kubwa  hasa kwa wateja wa itel S16, A56 na A35.
“Kuanzia sasa tunapozungumza mteja aliyenunua S16, A56 au A35 ataingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda zawadi kubwa kwa kupatiwa vocha maalumu ambapo droo itachezeshwa mara tatu na kila droo itakuwa na zawadi kubwa na droo ya kwanza itachezeshwa Februari 13, droo ya pili itachezeshwa Februari 23 na ya tatu ni Februari 27” Amesema Wolle.


Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa muda wa mwezi mmoja pia itafanyika kwenye kurasa za  za itel kwenye mitandao ya kijamii na wafuasi wa kurasa hizo watakaoshiriki watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post