Na Mwandishi Wetu.
Shirika la Usomaji kwa Kujifunza na Maendeleo-Soma kwa kushirikiana na mashirika mengine
yanayojihusisha na harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi kama vile Tanzania
Gender Network Program (TGNP), Woman Funds Tanzania (WFT), WAJIKI, VICOBA na
Msichana Initiatives inaratibu mradi ujulikanao kama TAPO Habari na Mshikamano Hub na
MOBOSOKO.
Mradi huu umebuni mfumo utakaowezesha katika kutetea
Wanawake/Wasichana kutoa taarifa mbali mbali kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
kwa wanawake wakati wa mlipuko wa COVID-19 na hata baada ya mlipuko wa COVID-19 kwa
kutumia teknologia ya simu za mkononi ijulikanayo kama Mshikamano Hotline. Vile vile, Soma
inatumia teknologia hiyo hiyo kuboresha mfumo wa upatikanaji wa mahitaji ya nyumbani kwa
kuwezesha soko kupitia simu ya mkononi, yaani MOBOSOKO App ili kukwepa misongamano
wakati wa mlipoko wa COVID-19 na hata baada ya mlipuko. Jukwaa hili litawezesha mizunguko
wakati wa marufuku ya kutotoka nje na umbali wa kijamii huku likiwezesha taarifa za siri kuhusu
uonevu wowote wa kijinsia.
"Katika jukwa ili tumeona nchi nyingi za Kiafrika na nyinginezo tumeona majanga yanapotokea watu wanajawa na hofu na wengine ukaa nyumbani na ukatili uongezeka na kuripoti hayo manyanyaso na ukatili huwa ngumu kwasababu hawawezi kutembea kwa uhuru kwahiyo kupitia simu za mkononi watu wataweza kuripoti masuala hayo kwa urahisi zaidi" , Alisema Bi. Debele Kitunga Mkuuwa Taasisi ya SOMA.
Hii leo Soma inaendesha mafunzo juu ya namna ya kutumia programu ya Mshikamano Hotline
pamoja na MOBOSOKO App. Mafunzo haya yanalenga kuongeza ufahamu juu ya namna ya
kutumia programu ya Mshikamano Hotline na MOBOSOKO App, kutengeneza nafasi ya
kushirikishana changamoto na mafanikio ya kifeminia wakati wa mlipuko wa COVID-19,
Kukusanya na kueneza mipango/hatua zilizichukuliwa na wanachama wa TFMB wakati wa
mlipuko wa COVID-19 na baada, Kujenga mfumo wa umoja na usaidiano kwa wanawake kwa
ajili ya usaidizi, kushirikishana na mwongozo.
Mafunzo haya yanafanyika TGNP,barabara ya mabibo, karibu na chuo cha NIT (National
institute of Transportation) kuanzia saa saa 3 asubuhi hadi saa 9 jioni.