FEPT wajipanga kuifanya Arusha ya Kijani


Na Mwandishi wetu, Arusha

SHIRIKA lisilo la kiserikali la mazingira foundation for Environmental Protection in Tanzania  (FEPT)  limejipanga kubadilisha taswira ya mji wa Arusha kwa kupanda miti zaidi ya 5000 katika maeneo ya wazi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa shirika Hilo Peter Mhagama wakati wa zoezi la kupanda miti katika kata ya Murieti lililofanywa  na shirika Hilo chini ya ufadhili wa  ubalozi wa Canada nchini.

Mhagama  amesema wameanza na zoezi hilo kwenye kata hiyo baada ya kuona eneo kubwa lipo wazi.

Alisema maeneo waliotoa kupaumbele kwenye upandaji miti hiyo katika kata ya Murieti  ni kwenye shule za sekondari na msingi za serikali,zahanati,vituo vya afya na ofisi za serikali ya mtaa zote.

"Lakini tumeona vema tuwagawie wananchi miti ili kila mmoja akapande nyumbani kwake na kuitunza tukiamini mwisho wa siku Arusha itakuwa ya kijani,"alisema.

Alisema zoezi la upandaji miti ni endelevu na watakapomaliza kwenye kata hiyo watahamia kata zingine zenye upungufu wa miti ili kupendezesha mkoa huo.

Afisa Tarafa ya Elerai Tito Cholobi aliomba shirika hilo kujikita kwenye ugawaji miti mitano kwa kila familiya kila mwaka  ili kutimiza lengo lao la kugeuza Arusha ya kijani.

Aliomba  kila mdau wa mazingira kuhakikisha miti inayopandwa ianatunzwa ili lengo la kupendezesha Arusha litimie.

"Nawaomba wananchi pandeni miti kwa wingi sababu miti ni mtaji mzuri bata ukipanda baada ya miaka miatatu au minne unabadilika na kukuletea fedha lakini ineta hewa nzuri na kuboresha mazingira,"alisema.

Diwani wa Kata ya Murieti, Francis Mbise alisema miti hiyo imepelekwa wakati muafaka nakipindi cha mvua na kushukuru kwa msaada huo, ambao utabadilisha mazingira yao ambayo  nyumba nyingi zipo wazi sababu ya ukosefu wa miti hasa maeneo ya mlimani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post