Kanisa Katoliki 'Moyo safi' laokoa 47 wanaoishi bila ndoa

Lafungisha ndoa Masuria 47, Kati ya 511

Na Seif Mangwangi, APC Blog Arusha

KANISA katoliki parokia ya Moyo Safi Unga limited iliyoko katika Jimbo kuu Katoliki Arusha limeingia katika historia baada ya kufungisha ndoa masuria 47 kati ya 511 wanaoishi bila ndoa katika parokia hiyo.

Akizungumza wakati wa kuwapatia sakramenti takatifu ya ndoa hiyo ya masuria Paroko wa Parokia hiyo Padre Festus Mangwangi amesema parokia hiyo imeingia katika historia kwa kuwapatia sakramenti hiyo takatifu waumini wengi kwa mpigo Jambo ambalo hutokea Mara chache Sana.

Kwa mujibu wa kanisa Katoliki, ndoa ya masuria hufungishwa kwa waumini wa dhehebu la kikatoliki dhidi ya wachumba zao kutoka katika dini na madhehebu mengine ambapo kila mmoja atakuwa akiabudu dhehebu lake na mmoja wa wanandoa anayetokana na kanisa Katoliki huruhusiwa kupata huduma zote za kikatoliki Kama mkristo.

Miongoni mwa ndoa zilizofungwa katika hafla hiyo ni pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kufungishwa ndoa na muumini wa kanisa hilo Katoliki aliyekuwa ametengwa na kanisa kwa zaidi ya miaka sita baada ya kufunga ndoa ya kiislam na baadae kuamua kurejea kanisani.

Padre Mangwangi amesema kuwa baada ya yeye na wasaidizi wake kupewa jukumu la kusimamia parokia hiyo waliamua kufanya sensa ya kujua idadi ya waumini wanaoishi bila ya kuwa na ndoa na kugundua kuwepo kwa idadi kubwa ya kada hiyo na wengi wao walilazimika kutofika kanisani baada ya kutengwa kwa kosa hilo.

“Tulipoingia mwezi Januari mwaka huu,tuliamua kuendeleza kile ambacho watangulizi wetu walifanya cha kukuza imani , lakini katika kukuza imani tuligundua kuwa kwenye parokia yetu tuna baadhi ya waumini ambao hawajafunga ndoa.

Na kuongeza" Kwa kushirikiana na kamati tendaji ya parokia tulifanya sensa nakupata waumini 511 ambao hawajafunga ndoa na hapohapo tukajiwekea  malengo ya kuhakikisha baada ya miaka miwili watu wote hawa wawe wametoka kwenye usuria na kufunga ndoa ili kanisa liwatambue.  

“ Leo hii waliofunga ndoa ni 47 na miongoni mwao wamefunga ndoa ya kikatoliki, lakini pia wapo  waliofunga ndoa ya mseto kwa maana kuwa mmoja anaendelea kubaki kwenye dini yake, sisi kama kanisa tunatamani watu waishi maisha ya ndoa,”alisema.

Ametoa wito kwa waumini wengine ambao bado hawajafunga ndoa kuacha tabia hiyo na badala yake wafike kanisani kuomba msamaha na kanisa litawafungisha ndoa ili waendelee kusali na kuabudu Kama ilivyoelekezwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post