WAFANYABIASHARA WA CEMENT WAPEWA ONYO KALI.

 NA AMINA SAID,TANGA.


MKUU wa mkoa wa Tanga Martine Shigella ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wa Cement kwa yeyote atakaepandisha bei atakiona Cha Moto.


Hayo ameyazungumza baada ya kutembelea viwanda vya Simba cement pamoja na Kilimanjaro cement kutaka kujua hali ya uzalishwaji wa bidhaa hiyo pamoja na bei za cement zinazouzwa viwandani hapo.


Shigella alisema kuwa amefarijika sana kwa sababu bei ya uzalishaji na bei ambayo inauzwa hapo  viwandani Bado haijabdilika  hiyo matarajio yao kwa wafanya biashara , wanunuzi pamoja na wasafirishaji ni kutokupandisha bei inatakiwa ibaki ileile iliyokuwa ikiuzwa katika kipindi Cha miezi mitatu nyuma iliyopita.


" Kwa hiyo nikiona au kusikia Kuna cement inapandishwa bei katika jiji letu la Tanga basi huyo mfanya biashara ajiandae kufanya biashara nyingine au atafute sehemu nyingine ya kufanyia biashara" alisema Shigella.


Aidha aliwataka wakuu wa wilaya ,wakurugenzi,maafisa biashara watendaji wa kata pamoja na maafisa tarafa watembelee maeneo yote ambayo biashara biashara ya cement inafanyika ili kuhakikisha kwamba bei ya cement inabaki ileile waliokuwa wakiuza katika kipindi chote Cha nyuma.


" Na yeyote atakae kuwa anakwenda kinyume maafisa biashara chukueni hatua ikiwa ni pamoja na kuwanyima leseni ili waweze kufanya shughuli nyingine ambazo wanataka kuzifanya " alifafanua Shigella.


Shigella alisema kuwa wao Kama Serikali wapo tayari kuwapa ushirikiano kwa viwanda hata Kama wapo tayari kuendelea kupanua wigo wa uzalishaji katika mkoa wa Tanga kwani matumizi ya cement kwa sasa ni makubwa sana hivyo wao Kama Mkoa wapo tayari kuwapa ushirikiano ili hatimae waweze kuongeza uzalishaji na baadae tuweze kuondokana na kero zinazowapata.


Kwa upande wake msimamizi mkuu wa fedha kiwanda Cha Kilimanjaro Filbert Mshange amesema kuwa kwa upande wa bei ya cement haijabadilika kwa muda mrefu labda bei iwe imebadilika kutoka kwa wale wanaonunua lakini kwa wao bei ya viwandani bado haijabadilika.


Mshange amesema kuwa kwa being ya kiwandani kwa ndani ya Tanga inauzwa sh.11600 na haijabadilika na kwa wale waliopo nje ya Tanga bei ya kiwandani ni sh. 10600 na hizo ndio bei zao za viwandani na hazijapanda.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post