MBUNGE ABOOD AANZA AWAMU KWA KASI YA AJABU, SHUHUDIA HAPA

 Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Leo ameendelea kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Morogoro Mjini ofisini kwake.  Amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kushughulika nazo Kama ifuatavyo:-1. Amesaidia kuwalipia wanafunzi wa Vyuo mbalimbali 24 jumla ya Tshs Milioni 14.3 kwa ajili ya Ada, Makazi, Nauli n.k ili waweze kusoma Kama alivyowaahidi kipindi Cha Kampeni.

2. Amesaidia Vifaa wanafunzi mbalimbali wa Shule za Sekondari na Msingi  Kama Uniform, Viatu, Mabegi na Madaftari vyenye thamani ya Tshs Milioni 3.63. Kuwaandikia Barua katika Hospital ya Rufaa Mkoa wa Morogoro wananchi 7 wenye matatizo mbalimbali ili waweze kupata Tiba Kisha bili yote ya gaharama za matibabu iletwe kwa Mheshimiwa Mbunge alipie.

4. Kuwalipia Bima za Afya Wakina Mama 12.

5.Amesaidia mitaji Vikundi 8 kila Kikundi laki 8 jumla ya Tshs Milioni Milioni 6.4 na mtaji kwa kina mama wauza mboga mboga mmoja mmoja kila mmoja Tshs 50,000 jumla Wakina Mama 32 wamesaidiwa jumla Tshs Milioni 1.6Katika siku ya leo kutekeleza Ahadi zake Mheshimiwa Abood ametumia Milioni 31.3 mfukoni mwake kusaidia masuala hayo kwa Wananchi wake. Aidha Mheshimiwa Abood ameahidi kuwahudumia Wananchi wake kwa kadri atakavyojaaliwa, Pia amewasihi Wananchi kuongeza juhudi katika kuunda Vikundi na kushiriki kikamilifu kwenye Shughuli za Uzalishaji.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post