CORONA YAPIGA HODI KUMBI ZA STAREHE, ZAAMUA KUPUNGUZA IDADI YA WATEJA

 


Na Mwandishi Wetu, Arusha.

Elimu ya afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa COVID-19 imeonesha kuzaa matunda baada ya wafanyabiashara wa kumbi za starehe kuamua kupunguza idadi ya wateja wanaoingia katika kumbi hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasimamizi wa kumbi hizo wamesema lengo la kufanya hivyo linatokana na maagizo yaliyotelwa na serikali juu ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuepuka misongamano isiyokuwa na lazima.

Wamesema hatua hiyo haijaathiri biashara kwani wanaendelea kutoa burudani kwa wateja wao kama kawaida na kwamba kilichobadilika na idadi ya watu hivyo kuwataka wateja kukubaliana na mabadiliko hayo.

Msimamizi wa ukumbi wa mziki wa Orstrich uliopo Kijenge, Mathias Chuwa wamesema ukumbi wake unauwezo wa kubeba watu mia moja kwa siku na siku za mziki walikuwa wakipata wateja kati ya 60-80.

Anaendelea kusema kuwa baada ya kuzuka kwa ugionjwa huo wameamua kuchukua watu wasizidi 50 lengo ni kulinda afya za wateja wake ikiwa ni pamoja watu wanaowazunguka.

“Licha ya kuwa hatuwezi kupata pesa au faida kama mwanzoni, lakini afya ya mwanadamu ni kitu cha muhimu zaidi ya pesa, hivyo sisi kwa hiari yetu tumeamua kuchukua tahadhari ya kupunguza idadi ya watu wanaingia klabuni siku za mziki” Alisema Chuwa.

Mmoja wa wasimamizi wa klabu ya Mjengoni amesema eneo lao ni kubwa na kwamba wateja wanapata nafasi wakati wa kucheza na hata kukaa hivyo bado hawajafikiria kupunguza idadi kwa kuwa eneo lao ni rafiki.

“Kama unavyoona eneo letu ni rafiki, lina ukubwa wa kutosha, lina uwazi pia, hewa ya kutosha, hivyo kuhusu kupunguza idadi bado hatujafikiria kwa sababu bado hatujapata wateja wengi wa kutuzidi, ikitokea tutafanya hivyo (kupunguza)” Alisema meneja huyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post