WAKULIMA MBARALI WAPEWA MBINU ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJIMhandisi Karoli Lihala akijibu swali kutoka kwa katibu wa Skimu ya umwagiliaji Isenyela Bw. Samweli Ngeve wakati wa Mafunzo Chimala Wilayani Mbarali Leo.

Baadhi ya Wakulima katika picha wakisikiliza mada
 

Na Mwandishi Wetu, Chimala Mbarali
 

Wakulima katika Skimu ya Isenyela wamepewa mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika kilimo cha umwagiliaji katika siku nyingine ya mafunzo kwa wakulima hao.


Akitoa moja ya mada mhandisi Karoli Lihala kutoka Wilayani Mbarali amewaeleza wakulima hao kuwa,ujenzi wa tuta katika njia ya kupeleka maji mashambani ni njia nzuri ya kuimairisha sehemu ya juu ya mto.

Alisema kuwa, kusakafiwa kwa mifereji na kujengwa kwa makaravati kunaweza kuimarisha zaidi skimu hizo.

Aliongeza kwa kusema kuwa kabla ya miundombinu ya umwagiliaji kuboreshwa na serikali “kwa sasa wakulima anaweza kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kutoa mchanga katika mto, kulinda vyanzo vya maji, kutoa magugu maji na kutofanya shughuli za kibinadamu kama kilimo katika vyanzo vya maji.” Alisisitiza

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post