WANA CCM KATA YA OSUNYAI WAPEWA SOMODiwani mteule kata ya Olasiti, Christopher Salvatory 


Na Mwandishi wetu Arusha

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi kata ya osunyai jijini hapa wametakiwa kutekeleza kwa vitendo ahadi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na chama hicho lakini pia kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa njia ya utekelezaji wa ahadi hizo.

Kwa sasa Chama Cha Mapinduzi hususani kwa mkoa wa Arusha kimefanikiwa kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha mapinduzi katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015 ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, barabara, maji na kuwawezesha wananchi wa Arusha kiuchumi.

Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Christopher Salvatory  ambaye ni mgombea mteule wa udiwani kata ya Osunyai jijini Arusha alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu, CCM itatoa ilani yake ambayo kila mteule atapaswa kuifuata na hivyo kutoa wito kwa kila mwana CCM kutekeleza ilani hiyo itakapozinduliwa rasmi wakati wa kampeni.

Amefafanua kuwa kwa kupitia nuru na uwajibikaji wa Raisi ,Magufuli ni wazi kuwa kila mgombea ambaye anawakilisha chama cha mapinduzi anatakiwa kuwa mfano na kuahidi kuwa yeye atakapochaguliwa kuwa Diwani atatekeleza ilani ya CCM.

" Rais wetu ameonesha uzalendo mkubwa sana na sisi kama wadau tunatakiwa kuhakikisha tunamuunga mkono kwa kuonyesha  uwajibikaji na usimamizi wa miradi mbalimbali na hii itasaidia kuondolewa kwa na changamoto lukuki ambazo bado zinawakabili wananchi wetu,"aliongeza

Katika hatua nyingine mgombea huyo alisema kuwa CCM imempa heshima kubwa sana ya kuweza kupeperusha bendera ya kata hiyo ya Osunyai lakini pia ana mpango wa kuhakikisha kuwa anatatua changamoto zikiwemo za miundombinu imara ndani ya kata hiyo

Alihitimisha kwa kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuweza kutafuta kura kwa kishindo za wagombea kuanzia ngazi ya udiwani na Urais.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post