MAAFISA UGANI ARUSHA WAPEWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA NZIGE

 

Na Mwandishi wetu Arusha

Shirika la chakula duniani (FAO) kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo wamefanikiwa kutoa mafunzo ya kupambana na nzige  wa jangwani kwa maafisa ugani 42 wa mkoa wa Arusha lengo likiwa ni kujiandaa kupambana na nzige ambao hufanya uharibifu wa mazao na mimea mbalimbali.

Akizungumza mapema jana wilayani Monduli mara baada ya kufunga mafunzo kwa maafisa ugani wa wilaya ya Monduli Afisa afya ya mimea kutoka FAO, Mushobozi Baitani alisema kuwa tahadhari ya Nzige hao ni muhimu kuchukuliwa

Baitani alisema kuwa janga la Nzige ni janga ambalo ni baya sana na linaathari kubwa sana kwenye jamii ndio sababu wameanza kuchukua tahadhari kwa kuanza kuwapa mafunzo wataalamu hao wa Mkoa wa Arusha

Alidai kuwa Nzige wanapovamia mahali huwa wanatabia ya kuharibu vyakula,mazao,pamoja na malisho mbalimbali ya mifugo jambo ambalo linasababisha ukame kwenye jamii husika ambayo hutegemea zaidi kilimo

"Athari za Nzige hawa wa jangwani kwa kweli ni kubwa sana na madhara yake ni makubwa sana sasa nchi kama Tanzania tayari tumeshaanza kuchukua tahadhari kwa kutoa mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na Nzige hao endapo kama watavamia maeneo mbalimbali"aliongeza

Katika hatua nyingine alisema kuwa jitihada mbalimbali ambazo wamezifanya ni pamoja na kutoa elimu sanjari na vitendea kazi kwa maafisa ugani hao ili endapo kama Nzige hao wa jangwani watawasili waweze kukabiliana nao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kiangamiza kizazi chao chote.

Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa nchi ya Tanzania mpaka sasa haijavamiwa na nzige hao wa jangwa ambao wametokea ukanda wa jangwa la sahara wakaingia somalia na kisha kuingia nchi za kenya na uganda

Alidai kuwa upepo wa Nzige hao wa jangwani upo nchini kenya na uganda lakini huenda ifikapo November mwaka huu upepo ukabadili njia na kisha tatizo la nzige kuwa limekwisha kabisa kwa kuwa kizazi cha kwanza kilishamalizika

Alihitimisha kwa kusema kuwa Nzige hao sio janga jepesi kabisa hivyo basi maafisa hao ugani wanatakiwa kutumia mafunzo hayo vyema lakini pia FAO kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo wanampango wa kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa ugani hasa wa mikoa ya mipakani kwa ajili ya tahadhari zaidi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post