DR MWINYI APITISHWA URAIS ZANZIBAR


Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi Kuwa Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu Oktoba 2020.

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya Taifa ya  CCM Spika Job Ndugai, amesema waliopigiwa kura ni Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16, Dkt Khalid Salum aliyepata 19 na Dkt. Hussein Mwinyi  aliyepata kura 129 sawa na asimilia 78.65 na hivyo kumfanya Dkt. Hussein Mwinyi kuchangulia kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kutagazwa kuwa mshindi Dkt. Mwinyi amesema kuwa amepewa heshima kubwa kwa kupata kura 129 na hiyo inaonyesha imani ya watu waliyonayo kwakwe na  kuahidi kuwa atafanya kazi kwa kulitumikia Taifa kwa uwezo wake wote.

"kinachonipa faraja ni kwamba tulikuwa 32 na hatimaye sasa niko mimi wezangu weote wako tayari kushirikiana nami kwa sasa hakuna timu Miwnyi wala timu nyingine bali kuna timu ya chama cha mapinduzi" amesema Mwinyi

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa umefanyika CCM makao makuu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dkt. John Magufuli

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post