SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU KIGOMA LAKABIDHI VIFAA VYA HUDUMA YA DAMU NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILION 67

Wa katikati ni Meneja wa mradi wa damu salama Redcross Kigoma akitoa maelekezo ya matumizi ya vitu vya kulalia wakati wa kuchangia damu kwa mganga mfawidhi wa mkoa Dkt. Osimundi Dyegula
Wa kwanza kushoto mwenye suti la blue ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Kigoma Dkt Saimon Chacha akipokea moja ya kifaa kutoka kwa mwenyekiti wa Redcross Kigoma Musa Kifyumu
Na Diana Rubanguka,  Kigoma.

Shirika la msalaba mwekundu Tanzania red cross Mkoa wa Kigoma limetoa msaada wa vifaa tiba vya damu salama vyenye thamani ya zaidi ya shilingi niliona 68 ikiwa ni sehemu ya kuchangia huduma za kijamii katika mradi huo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma, mwenyekiti wa shirika la Redcross Mkoa wa Kigoma Musa Kifyumu alisema shirika hilo lilitembelea vituo vya damu ya kibaoni changamoto mbalimbali ambazo nimekua chachu ya kutoa vifaa hivyo.

"tulibaini ukosefu wa vitu vya kulalia wakati wa kuchangia damu, vifaa vya kuhifadhia damu, elimu kwa watoe huduma pamoja na umeme wa dharula hivyo tukaona tuchangie katika changamoto hizo" alisema kifyumu.

Mganga MKuu wa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Kigoma Dkt. Saimon Chacha alishukuru shirika hilo kwa kutambua changamoto hizo za vituo vya damu na kuzifanyia kazi.

Dkt. Chacha alitoa wito kwa watumishi wa afya kuthamini na kutunza mchango huo kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya kutotunza na kujali vifaa vinavyotolewa na wadau kwa kutovinea uchungu.

Hata hivyo ameiomba Redcross kushirikiana na serikali katika kutoa huduma itakapohitajika  kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Korona katika nchi mbalimbali ambapo Tanzania sio hawanga lakini shirika la World Health organisation WHO limethibitisha uwepo wa mgonjwa mmoja nchini Kongo nchi ambayo ni jirani na Mkoa wa Kigoma kwa kuwa muingiliano wa shughuli za  kiuchumi ni mkubwa hivyo lolote linaweza kutokea.

Awali Meneja mradi wa damu salama Redcross Kigoma Abich Maramba alivitaja vifaa hivyo kuwa ni jokofu la kuhifadhia damu, vitanda 16 vya kulalia wakati wa kuchangia damu, vibebeo 8 vya sampuli ya damu, vibebeo 10 vya damu, Mizani mitatu ya kupima damu na mmoja wa kupima uzito. 

Sambamba na hivyo wametoa computa mpakato moja, printa, computa ya mezani, Viti vya ofisini vitano, jenerata kubwa la umeme pamoja, vitanda viwili vya kulalia wakati wa kuchangia damu pamoja na box la vifaa vya maabara vya dharula.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post