
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushiriikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
amesema kuwa mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 17 Machi 2020
ambapo utatanguliwa na mkutano wa wataalamu pamoja na Makatibu Wakuu na
kufuatiwa na mkutano wa mawaziri tarehe 16 - 17 Machi, 2020.
"Pamoja
na mambo mengine, mkutano huu utahusisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango pamoja na
Mawaziri wa Viwanda na Biashara," Amesema Prof. Kabudi
Waziri
Kabudi amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na Mawaziri 16 kutoka Nchi
wanachama wa SADC za Angola, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Comoro,
Lesotho, Mauritius, Madagascar, Kongo DRC, Shelisheli, Msumbiji, Afrika
Kusini, Tanzania, Malawi, Botswana pamoja na Eswatini)
Aidha,
Kwa mujibu wa Mhe. Waziri Kabudi, Mkutano huo utakuwa mkutano wa
kwanzawa SADC wa Baraza la Mawaziri kuendeshwa kwa lugha ya Kiswahili
baada ya lugha hiyo kuwa miongoni mwa lugha rasmi za Jumuiya hiyo.
Prof.
Kabudi aliongeza kuwa, mkutano huo utajadili masuala mbalimbali muhimu
kwa mustakabali wa maendeleo na ustawi wa nchi wananchama wa SADC.
"Mktano
huu utapokea taarifa na kutolea maelekezo taarifa za vikao mbalimbali
vya kisekta vya kamati za mawaziri ambavyo vimefanyika nchini tangu
Septemba 2019," Ameongeza Prof. Kabudi.