Makongolosi wafurahia ujio wa shule ya mchepuo wa kingereza

Mkurugenzi wa Shule ya Holyland Pre & Primary school iliyopo Makongorosi wilayani Chunya mkoani Mbeya,Lawena Nsonda maarufu kwa jina la Baba mzazi  wakiwa na mmoja wa walimu wa shule hiyo Tracila Joachim wakiwaangalia baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakicheza mchezo wa kubembea wakati wa mapumziko.(Picha na Joachim Nyambo)
Na Joachim Nyambo,Chunya.
WAKAZI katika mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya wamesema kufunguliwa kwa shule ya mchepuo wa kingereza kwenye eneo lao kumeanza kuleta mwamko na hamasa kwa wazazi kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto wao kwenye shughuli za machimbo na sasa wanaona elimu inaweza kuwakomboa zaidi.
Wakazi hao wamesema wazazi wameanza kushawishika baada ya kuona watoto wachache wanaosoma katika shule ya mchepuo wa kingereza  ya Holyland Pre & Primary school iliyopo katika mji wao wanaonesha uwezo wa kuongea kingereza na kuona kama iwapo wataendelea kutochangamkia fursa za elimu nchini watoto wao wanaweza kuendelea kubaki vibarua kwa wasomi.
Wakizungumza na waandishi wa habari wanaofuatilia Masuala ya elimu na changamoto zake kwa watoto kwenye maeneo yaliyo na machimbo ya madini wakazi hao wamesema jitihada za wadau mbalimbali katika kuchangia sekta ya Elimu zinahitajika ili kuwakomboa watoto waishio kwenye maeneo ya migoni.
Mmoja wa wakazi hao Listaa Rashid Masumaye alisema ufunguaji wa shule bora na za kisasa jirani na maeneo ya wakazi waishio karibu na zinakofanyika shughuli za machimbo ni moja kati vishawishi vikibwa vinavyoweza kuwahamasisha wazazi kuona elimu kwa watoto wao inapaswa ipewe kipaumbele kwanza kabla ya shughuli zao.
 “Mazingira yenye kumtamanisha mzazi yanaweza kumsaidia kuwa na tama ya kuiga ili watoto wake waonekane wa kitofauti na wa wenzake.Unajua hapa Makongolosi awali tulikuwa kama tunaishi kwa mazoea kwa kuona mbona hata waliosoma wanafanana na watoto wetu tu wanashinda wote kwenye kuchimba.Lakini kumbe ilikuwa ni kwakuwa hatukuona utofauti wa elimu inayoweza kutolewa.”
“Ilikuwa ajabu kuona mtu akiongea kingereza..Kuna mahafali moja ilifanyika hapa..ilileta mwamko mkubwa sana katika Makongolosi..kwamba hivi kuna uwezekano mtoto mdogo namna hii kuongea kingereza…Hapa imekuwa kama kituo cha utalii…vitoto vidogo viliwaacha watu mdomo wazi..Kilichofuata sasa kila mzazi hata familia ambazo zimekuwa nyuma kupeleka watoto shule wakaanza kusema lazima tujitahidi watoto wasome.Vinginevyo watoto wetu watakuja kubaki vibarua wa hawa wanaochangamkia elimu.”alisema Rashid.
Mkazi huyo aliwasihi wazazi kutumia fursa ya uwepo wa sifa kubwa ya kielimu kwa mkoa wa Mbeya kwa kubadilika na kuendana na maisha ya kisasa kwa kuwapeleka watoto wapate elimu jambo alilosema litakuja kuwasaidia pia katika shughuli zao za uchimbaji kwakuwa watakuwa na utaalamu zaidi ya wazazi wao.
Mkazi mwingine Edith Jairos alikiri kuwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo wakazi wa wilaya ya Chunya walikimbilia kazi za uchimbaji na kusahau kupeleka watoto shuleni,utandawazi unaonekana kuwaunganisha wakazi hao watu wa maeneo mengine hatua inayowasukuma kuanza nao kutafuta shule zitakazowawezesha watoto wao kustahimili ushindani wa soko la ajira.
Edith alisema wapo wachimbaji ambao hivi sasa wamefikia hatua ya kufanya mashindano kwa kila mmoja kutamba kwa kumpeleka mtoto wake kwenye shule inayofanya vizuri zidi ya wenzie hatua aliyosema kwa miaka ya nyuma ilikuwa ni ndoto.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Shule ya Holyland Pre & Primary school,Lawena Nsonda alisema wakazi wa mji wa Makongolosi na maeneo ya jirani ndiyo waliosababisha akabadili mawazo badala ya kufungua Hospitali akaamua iwe shule ya mchepuo wa kingereza kulingana na mahitaji yaliyokuwepo.
Nsonda alisema awali yeye na rafiki zake madaktari ambao wengi wanafanya shughuli zao katika Hospitali zilzopo jijini Mbeya walikuwa na mpango wa kufungua hospitali ili iweze kutoa huduma za matibabu kwa wakazi wa maeneo hao ambao wengi wao shughuli zao ni za machimbo ya madini na hasa dhahabu lakini baadaye wakazi walimfuata na kutana iwe shule.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post