Wadau watakiwa kushikamana kuwalinda watoto Chunya

Na Joachim Nyambo,Chunya.
 WADAU wilayani Chunya mkoani Mbeya wametakiwa kushikamana kwa pamoja ili kudhibiti matukio ya ukatili dhidi ya watoto yanayoonekana kushamiri wilayani hapa huku watekelezaji wa matukio hayo wakiwa ni watu wa karibu wakiwemo wazazi.
 Image result for ukatili dhidi ya watoto
Katika siku za hivi karibuni wilaya ya Chunya imekumbwa na matukio kadhaa ya ukatili dhidi ya watoto na wengi wa wahanga wa matukio hayo ni watot walio na umri wa chini ya miaka mitano wanaohitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa jamii inayowazunguka.

Ofisi ya Ustawi wa jamii wilayani hapa imekiri kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimekithiri wilayani hapa na sasa vinatishia maisha ya watoto na kuwa jitihada za pamoja zinahitajika ili kuwanusuru na vitendo hivyo.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chunya, Theresia Mwendapole alibainisha hayo alipozungumza na mwandishi wetu juu ya tukio la hivi karibuni la mwanamke mmoja wilayani hapa kumchomo moto makalio mwanaye wa kike wa kumzaa mwenye umri wa miaka miwili na miezi saba kutokana na kile alichodai mtoto huyo kuwa na tabia ya kujisaidia hovyo(kujinyea).

Kwa mujibu wa Theresia mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Agatha Julius(21) mkazi wa kata ya Itewe wilayani hapa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa wakati mtoto akiendelea kupata matibabu hospitali ya wilaya na atakapopona mtuhumiwa atakabidhiwa Polisi ili hatua zaidi za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yake.

Afisa huyo alisema tukio hilo lilitokea Februari 10 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi nyumbani kwa mzazi huyo katili aliyedai kuchoshwa na tabia za mwanaye za kwenda haja hovyo.


Theresia alisema baada ya ofisi yake kupata taarifa za tukio hilo kutoka kwa majirani wema waliolibaini walifika nyumbani ambapo walimchukua na kumuwahisha katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya alikolazwa kwaajili ya matibabu.


Hata hivyo afisa huyo anasema kinachomsikitisha ni kuwa licha ya ofisi yake kutumia nguvu kubwa kutoa elimu kwa jamii juu ya malezi bora ya watoto hasa wadogo bado vitendo hivyo vinashamiri wilayani hapa.

"Hivi karibuni mwanamke mmoja alikamatwa kwa tuhuma za kumuua na kumzika porini mwanawe eneo la Igundu.Wilaya hii kila siku ukatili dhidi ya watoto wadogo unaongezeko"alisema Theresia.

Kwa upande wao baadhi ya majirani wa mama aliyemchoma moto makalio mwanaye akiwemo Kissa Kayuni walisema kitendo kilichofanywa na mama huyo si cha kiungwana hasa ikizingatiwa huyo ni mwanawe wa kumzaa.

Naye mjumbe wa Kamati ya usalama wa mtoto Wilaya ya Chunya Mchungaji Elisha Mwakabana alisema wazazi wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu kwa kuhudhuria nyumba za ibada ili watu waepukane na matendo maovu katika jamii.

Diwani wa Kata ya Itewe,Alex Kinyamagoha aliwaonya wananchi kuacha tabia za kujichukilia sheria mkononi kama alivyofanya mwanamke huyo kwani baadae wahanga wanaweza kulipiza kisasi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post