UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WAANZA KUPATIWA UFUMBUZI

Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Tatizo la Ukatili  dhidi ya   wanawake na watoto miongoni mwa jamii huenda likapatiwa ufumbuzi wa kudumu baada ya wizara ya katiba na sheria kuanza kuwapatia elimu viongozi wa dini na kimila ili waweze kuielimisha jamii kuhusu haki ya mwanamke na watoto.

Akiongea jijini Arusha naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo,Amon Mpanju alisema kuwa warsha hiyo  ya siku mbili imelenga kutambua haki ya mwanamke,haki za binadamu na haki za watoto ,walemavu na makundi mengine kuweza kuthaminiwa .

Alisema kuwa viongozi wa dini na Mila wanaushawishi mkubwa  katika jamii yao ,kuaminiwa hivyo hatua ya kupewa mafunzo hayo kutaisaidia serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto vinavyozidi kushamiri miongoni mwa jamii.

"Tumieni majukwaa yenu ya dini na  Mila kuisaidia serikali kutokomeza vitendo vya kikatili ,unyanyasaji dhidi ya wanawake ,watoto na walemavu ,najua mnamchango mkubwa sana kwa jamii myatumie mafunzo hayo kwenda kuielimisha jamii kwa kukemea hadharani" Alisema

Kwa upande wa viongozi wa dini akiwemo sheikh Hussein Junje na Mchungaji wa kanisa la Maranatha lililopo kwa Morombo jijini hapa ,mchungaji Sadick Kinanga walisema kuwa,watahakikisha mafunzo  hayo wanayopewa wanayatumia  kwenda kutoa elimu   juu ya haki za sheria dhidi ya wanawake na watoto na hatimaye kuweza kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi yao.

Hata hivyo walisema kuwa,wataweza kutumia nafasi zao kuhakikisha wanaelimisha jamii kupinga vita matukio  hayo ya ukatili wa kijinsia kwani bado yanaonekana kushamiri katika jamii inayotuzunguka.

Naye Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha ,Blandina Nkini alisema kuwa,tatizo la unyanyasaji  na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mkoani hapa bado linaendelea kushika kasi,hivyo uwepo wa mafunzo hayo kwa viongozi hao itasaidia sana kuibadilisha jamii kutambua umuhimu wa  kulinda na kuheshimu haki za wanawake, watoto na walemavuy.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na wizara ya sheria na katiba kwa kushirikiana na mkoa wa Arusha ambapo yamewashirikisha viongozi hao kutoka mikoa ya Arusha na Manyara .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post