Ubalozi wa Marekani Iraq na Kambi ya Jeshi Wapigwa Tena Kwa Makombora

Makombora manne leo hii yamevurumishwa karibu na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na kambi ya kijeshi ambayo inatumiwa na vikosi vya Marekani ndani la Ukanda wa Kijani. 

Hata hivyo hakuna athari kubwa zilizoripotiwa. Msemaji wa operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq, Kanali Myles B. Caggins, amesema mashambulizi hayo yalitokea majira ya tisa na nusu Alfajiri, na kuongeza kuwa yalipiga tu kambi inayohifadhi wanajeshi wa Marekani na wa muungano.

 Hata hivyo maafisa watatu wa usalama wa Iraq wamesema mawili kati ya makombora hayo yaliangukia katika eneo la ubalozi wa Marekani, wakati lingine likitua katika kambi ya jeshi la muungano.

 Maafisa hao wa Iraq waliyasema hayo kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuwa hawana mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post