MATUSI YAMKERA SAMATTA

Mshambuliaji wa klabu ya Aston villa na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ameeleza masikitiko yake kufuatia maoni yasiyoridhisha ya Watanzania katika mitandaao ya kijamii.Samatta amesema hayo kufuatia Watanzania kutoa maoni yasiyoridhisha yakiwemo matusi katika kurasa za klabu ya Aston Villa na kurasa za wachezaji wa timu hiyo, wakidai kuwa mchezaji wao hapewi nafasi nyingi uwanjani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Samatta ameandika, "mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika kurasa za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi".

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post