VODACOM YAFUNGIA LAINI ZA WATEJA 157,000

Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM,
WATEJA 157,00 wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wamefungiwa huduma zao kutokana na kushindwa kujisajili kwa kutumia alama za vidole.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi ametangaza uamuzi huo leo Januari 22, mwaka 2020 jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hatua hiyo Hendi amewaomba wateja wote waliofungiwa laini zao kutembelea vituo vya huduma au mawakala wa kampuni hiyo zaidi ya 35,000 nchini kusajili laini zao ili kuendelea kufurahia huduma za kampuni hiyo.
Amesema baadhi ya maduka yao kwenye miji mikubwa yatakuwa wazi Saa 24 ili kuhakikisha wateja wanaendelea kupatiwa huduma hususani kwa wenye vitambulisho vya taifa,” amesema Hendi.
Hatua hii inatokana na agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kuziagiza kampuni zote za simu nchini kuwafungia wateja ambao wameshindwa kusajili kwa kutumia alama za vidole ifikapo Januari 20, mwaka huu.
Amesema wateja walioathiriwa na zoezi hili ni wale tu waliopokea namba za vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA, lakini wameshindwa kujisajili kwa sababu moja au nyingine.
“Kwa kuwa zoezi hili ni endelevu, wateja wetu wote ambao hawajapata namba za utambulisho kutoka NIDA, waendelee na mchakato wa kupata namba hizo au vitambulisho vitakavyowawezesha kujisajili kwa kutumia alama za vidole na kuepuka usumbufu wa kufungiwa huduma,” amesema.
Pamoja na mambo mengine, Hendi amesema zoezi la usajili kwa alama za vidole litasaidia kupunguza idadi ya matapeli wanaosumbua wateja ambapo itarahisisha vyombo vya usalama kupambana na matukio hayo ya kitapeli.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare amesema kwa wale walioathiriwa na zoezi hili la kufungiwa wasiwe na wasiwasi kwa vile taarifa zao zitatunzwa kwa muda wa miezi sita ambapo wanatarajiwa wawe wamejisajili kwa alama za vidole. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post