Mashambulizi ya roketi yafanywa katika kambi ya jeshi ya Iraq Ambayo ni Makazi ya Wanajeshi wa Marekani

Jeshi la Iraq limesema karibu makombora sita yamerushwa katika kambi ya kijeshi ya Balad kaskazini mwa Mji Mkuu wa Baghdad leo na kuwajeruhi wanajeshi wanne wa Iraq. 

Kambi hiyo ambayo iko kilomita 80 kaskazini mwa mji huo mkuu ni makao ya majeshi ya Marekani pia ingawa kiasi kikubwa cha wanajeshi wa Marekani walikuwa washaondolewa na kupelekwa kwengine kutokana na mvutano unaozidi kati ya Marekani na Iran.

 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema ameghadhabishwa na ripoti za mashambulizi hayo. 

Taarifa kutoka kwa jeshi la Iraq imesema roketi nane zimerushwa katika kambi hiyo ya kijeshi jana na kuangukia katika njia ya ndege na lango la kambi hiyo. 

Hakuna aliyekiri kuhusika na mashambulizi hayo kufikia sasa. Hakuna aliyeuwawa katika mashambulizi hayo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post