Kamwelwe: Muda Wa Kusajili Laini Za Simu Hautaongezwa

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali haitaongeza muda wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole, huku akitahadharisha kuwa katika siku zilizosalia, kasi ya wizi wa kimtandao kupitia simu za mkononi imeongezeka.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu siku zilizobaki kabla ukomo wa siku 20 alizotoa Rais John Magufuli, haujawadia. Mwisho wa usajili ni Januari 20 mwaka huu.

“Kumejitokeza wizi wa kimtandao; wananchi tuwe macho sana tunapomalizia hizi siku zilizosalia kabla laini ambazo hazijasaliwa hazijazimwa. Watu wanatumia siku chache zilizosalia kuibia watu kwa kiwango cha juu; bila kuwa makini, watu tutaibiwa sana,” alihadharisha Waziri Kamwelwe.

Waandishi wa habari walipotaka kujua kama siku za usajili huo kwa alama za vidole zitaongezwa, waziri alisema: “Hakuna siku kuongezwa; siku za usajili hazitaongezwa.”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post