Breaking News : BASI LA BRIGHT LINE LAPATA AJALI SHINYANGA...KUNA VIFO NA MAJERUHI


Basi la Bright Line lenye namba za usajili T437DFJ lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Dodoma limepata ajali katika eneo la Isela barabara ya Shinyanga - Tinde baada ya dereva wa basi akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kusababisha kugonga gari dogo na kupinduka leo Jumatatu Januari 13,2020 majira ya saa nne asubuhi. 

Taarifa za awali zinasema kuwa watu wawili wamepoteza maisha na majeruhi kadhaa.
Tutawaletea taarifa kamili hivi pundeThis is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post