Mkurugenzi Same Awasimamishwa kazi Watumishi Wawili kwa Tuhuma za Rushwa

Na Ahmed Mahmoud,Killimanjaro.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annaclair Shija amewasimamisha watumishi wawili wa hospitali ya wilaya hiyo akiwemo  Afisa Tabibu kwa kudai na kupokea rushwa ya shs. 15,000/= kutoka kwa mama mwenye mtoto mchanga  mgonjwa wakike mwenye umri wa miezi mitano wa kijiji cha Vunta kilichopo ukanda wa milimani mwa wilaya hiyo.

 Shija amechukua hatua hiyo baada ya afisa tabibu huyo Kimweri kihiyo amesimamishwa kwa kumwandikia upasuaji mtoto huyo ambao hakustahili na kudai rushwa hiyo huku mlinzi daniel kihara  alimuuzia dawa kutoka bohari ya serikali kwashs. 4,500/ kwa mama wa mtoto huyo ambaye alistahili apewe mtoto wa miaka 12.

 Aidha amesema,  vitendo vya aina hiyo vimekuwa vikiidhalilisha serikaliambayo imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya dawa ambazo zinapatikana kwa asilimia 90 na kitendo cha kumwandikia dawa na upasuaji ambao hakustahili ni sawa mauaji .

Muuguzi wa hospitali hiyo bw  Fabian Bulili  amesema kuwa afisa tabibu huyo ambaye hakuwa kazini anaonyesha alikuwa na tabia ya kuwaandikia dawa wagonjwa kwa ushirikiano na watumishi wasio waaminifu na kujipatia fedha kuikosesha mapato halmashauri

Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo  eliabu mgonja wameipongeza hatua hiyo na kueleza kuwa watumishi wa aina hiyo wanastahili kufukuzwa kazi ili wananchi waendelee kupata huduma bora za afya bila kudaiwa rushwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post