WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUPATA CHETI CHA KUZALIWA BURE

Na.Farida Saidy,Morogoro

Wakala Wa Usajili Ufilisi Na Udhamini (RITA) Kupitia Wasajili Wa Huduma Ya Uandikishaji Watoto Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Wametakiwa  Kutofanya Urasimu wa kuwatoza  Watu Fedha kwa ajiri ya malipo ya ya cheti cha kuzaliwa,  Ikiwa Mkakati Uliopo sasa Ni Kusajiliwa Bure, Na Kwa Atakaebainika Kufanya Hivyo Hatua Kali za kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake.

Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Mororgoro Bw.Loata Ole Sanare Wakati Wa Ufunguzi Wa Semina Ya  Wakala Wa  Usajili Ufilisi Na Udhamini  (RITA)  Uliowahusisha Viongozi Mbalimbali Wa Kimkoa Wenye Dira Ya Kufikia Lengo La Kusajili Watoto Zaidi Y Asilimia 90 Ya Watoto Wote  Bure , Wenye Umri Chini Ya Miaka Mitano Mkoani Morogoro.

Kwa Upande Wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu  Kutoka RITA Bi.  Emmy Hudson  Amesema Ili Kukamilisha Majukumu Kwa Watendaji Kuhusu Mpango Huo,Wameandaa Mafunzo Kwa Wahusika Wote ,Wakiwemo Watumishi Sita Kutoka Kila Halmashauri  Mkoani  Morogoro ,Pamoja Na Mtumishi Mmoja Mmoja Kutoka Idara Ya Usalama Na Idara Ya Uhamiaji .

Nao Baadhi Ya Washiriki Wa Semina Hiyo Wakiwemo Viongozi Mbalimbali Wa Kiserikali Na Kidini Wameusifu Mpango Huo Wa  Usajili  Bure Wa Watoto Wenye Umri  Chini Ya Miaka Mitano Unaoendelea Kuifikia Mikoa Mbali Mbali Nchini Na Kusema Kuwa Utawasaidia Katika Kuharakisha Upatikanaji Wa Haraka Wa Vyeti Hivyo.

Ikumbukwe Kuwa  Kundi La Awali La Watoto  Walio Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Limekwishaanza  Utekelezaji Wake Ambapo Ni Mikoa Ya Mbeya  Songwe Mwanza Njombe Iringa  Geita  Shinyanga Lindi Mtwara Mara Simiyu Dodoma Na Singida Ambapo Kwa Sasa Ni Zamu Ya Morogoro Pamoja Na Pwani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post